Naibu
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura
akizungumza na waandishi wa habari wadau wa harakati za upatikanaji wa
lishe bora nchini na wahariri wa vyombo vya habari katika hafla ya
kuwatunuku tuzo waandishi bora wa masuala ya lishe nchini iliyofanyika
Jijini Dar es Salaam Novemba 22,2016.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Jukwaa la Lishe Tanzania(PANITA) Bw. Tumaini Mkindo
akielezea mikakati na utekelezaji wa mipango ya Jukwaa la Lishe Tanzania
katika kuboresha upatikanaji wa lishe bora nchini katika hafla ya
kuwatunuku tuzo waandishi bora wa masuala ya lishe nchini iliyofanyika
Jijini Dar es Salaam Novemba 22,2016.
Katibu wa
Jukwaa la Wahariri Tanzania Bw. Neville Meena akizungumza katika hafla
ya kuwatunuku tuzo waandishi bora wa masuala ya lishe nchini
iliyofanyika Jijini Dar es Salaam Novemba 22,2016.
Mwakilishi
wa Ubalozi wa Ireland na Irish Aid Bi. Neema Shosho akizungumza kwa
niaba ya ubalozi kuhusu masuala ya lishe katika hafla ya kuwatunuku tuzo
waandishi bora wa masuala ya lishe nchini iliyofanyika Jijini Dar es
Salaam Novemba 22,2016.
Naibu
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura
akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Lishe
Tanzania(PANITA) Bw. Tumaini Mkindo wakati wa hafla kuwatunuku tuzo
waandishi bora wa masuala ya lishe nchini iliyofanyika Jijini Dar es
Salaam Novemba 22,2016.
Naibu
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura
akikabidhi cheti zawadi ya tablet na Shillingi million 1.5 kwa Bi
Tumaini Msoyowa mshindi wa kwanza wa Shindano la mwandishi bora wa
habari zinazohusu lishe kutoka gazeti la Mwananchi katika hafla
iliyofanyika Jijini Dar es Salaam Novemba 22,2016.
Naibu
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura
akikabidhi cheti zawadi ya tablet na Shillingi million 1. Kwa mwakilishi
wa Bi Winny Itaeli wa mshindi wa pili wa Shindano la mwandishi bora wa
habari zinazohusu lishe kutoka gazeti la The Guardian katika hafla
iliyofanyika Jijini Dar es Salaam Novemba 22,2016.
Naibu
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura
akikabidhi cheti na Shillingi laki 5 kwa Bw. Gerald Kitabu mshindi wa
tatu wa Shindano la mwandishi bora wa habari zinazohusu lishe katika
hafla iliyofanyika Jijini Dar es Salaam Novemba 22,2016.
Washiriki
wa shindano la mwaandishi bora wa habari za masuala ya lishe pamoja na
wageni waalikwa wakifuatilia hotuba mbalimbali ikiwemo ya Naibu Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura wakati wa
hafla iliyofanyika Jijini Dar es Salaam Novemba 22,2016.
Naibu
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akiwa
katika picha ya pamoja na viongozi wa Jukwaa la Lishe Tanzania,
wahariri wa vyombo vya habari,waandishi wa habari washiriki na washindi
wa Shindano la mwandishi bora wa habari zinazohusu lishe katika hafla
iliyofanyika Jijini Dar es Salaam Novemba 22,2016. Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM.
Na Raymond Mushumbusi WHUSM
Serikali
imeahidi kutenga jumla ya Dola za kimarekani Millioni 115 kwa ajili ya
kuboresha lishe ikiwa ni mpango wa maendeleo wa miaka mitano 2016/2021
na mkakati wa kuboresha lishe kwa mwaka 2016/2021.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.
Anastazia Wambura alipokuwa akizungumza katika halfa ya kuwatunuku tuzo
waandishi bora wa habari zinazohusu lishe iliyofanyika leo Jijini Dar es
Salaam.
Mhe.
Anastazia Wambura ameongeza kuwa bado kumekuwa na changamoto katika
upatikanaji wa lishe bora nchini ikiwemo kuwepo kwa tamaduni mbalimbali
zinazonyima fursa kwa watoto na wakina mama kupata lishe iliyo bora.
“Serikali
imeingiza suala la lishe katika mpango wa maendeleo wa taifa wa miaka
mitano na katika kulitekeleza hili Serikali ya awamu ya Tano itatenga
dola million 115 kwa ajili ya mkakati wa kuboresha lishe nchini”
alisisitiza Mhe. Anastazia.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Lishe Tanzania(PANITA) Bw.
Tumaini Mkindo amesema kuwa hali ya lishe imeendelea kuimarika hasa kwa
miaka mitano iliyopita hili linadhihilisha kuwa mikakati thabiti iliyopo
imesaidia kwa asilimia kubwa kupambana na tatizo la ukosefu wa lishe
bora nchini.
Bw.
Mkindo ameipongeza Serikali kwa juhudu inazozichukua katika kupanga
mikakati na kuitekeleza katika suala la upatikanaji wa lishe bora nchini
ili kuondokana na suala la udumavu linaloleta athari kubwa katika
ukuaji wa Binadamu.
Ameongeza
kuwa Jukwaa la Lishe Tanzania litaendelea kushirikiana na Serikali na
wadau wengine katika harakati za upatikanaji wa lishe bora na kufikia
malengo ya Shirika la Afya Dunia (WHO) yaliyosainiwa na Tanzania
yahusuyo masuala ya lishe pamoja na kupunguza udumavu kwa asilimia 40
ifikapo mwaka 2025.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment