Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akiwasalimiana na viongozi wa
Wilaya katika eneo la mapokezi wakati wa ziara yake Wilayani hapo.
Nteghenjwa Hosseah , Monduli.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ameuagiza uongozi wa wilaya ya Monduli
Mkoani Arusha pamoja na baraza la madiwani la wilaya hiyo kuhakikisha
wanabadilisha umiliki wa shamba la Manyara ranch lenye ukubwa wa ekari
44,930 kutoka kwa taasisi ya Tanzania Land Conservation Trust{TLCT}
kwenda kwa wananchi wa vijiji viwili kama Rais wa awamu ya tatu Mhe.
Benjamini William Mkapa alivyoagiza.
Rc
Gambo alitoa agizo hilo katika mikutano ya hadhara iliyofanyika katika
kata ya Elesilalei na Makuyuni baada ya kutembelea miradi ya mamilioni
ya fedha iliyopo ndani ya shamba hilo inayofadhiliwa na African Wildlife
Foundation{AWF} na kuelezwa kero na changamoto zilizopo juu ya umiliki
wa shamba hilo kwa taasisi ya TLCT.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha akitoa maelekezo ya kubadilisha Hati ya Umiliki wa
shamba kutoka kwa TLCT kwenda kwa wananchi wa vijiji vya Elesilalei na
Ortukai.
Alisema
nyaraka zinaonyesha wazi kuwa Shamba hilo lilitolewa kwa wananchi wa
vijiji vya Elesilalei na Ortukai na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu mwaka
1999 kwa ajili ya kilimo na ufugaji lakini hilo halikufanyika badala
yake taasisi ya TLCT ikajimilikisha shamba hilo kinyume na maagizo.
Mkuu
huyo wa Mkoa alisema kutokana na hali hiyo ninawaagiza viongozi wote wa
wilaya ya Monduli wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo pamoja na baraza
la madiwani kuhakikisha ndani ya muda mfupi wanabadilisha umilikiwa wa
shamba hilo kutoka taasisi hiyo kwenda katika vijiji hivyo.
Gambo
alisema serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt John
Magufuli iko madarakani kwa ajili ya kuwahudumia wanyonge na watu wa
hali ya chini na kamwe haiwezi kuona baadhi ya watu fulani wananufaika
na rasilimali ya nchi kwa manufaa yao.
Meneja
wa Ranch hiyo Ndg. Fidelis Ole Kashe akiwasilisha taarifa ya Shamba
hilo kwenye Kikao maalum na Mkuu wa Mkoa wa Arusha pamoja na viongozi wa
Wilaya.
Alisema
TLCT inamiliki shamba hilo kinyume na maagizo kwani shamba hilo
lilipaswa kumilikiwa na vijiji hivyo kwa faida yao lakini walijitokeza
wataalamu wakabadilisha maelekezo hayo na kujimilikisha kitu ambacho
Serikali ya Awamu ya Tano haiwezi kulivumilia kamwe.
‘’Nimeagiza
umiliki wa shamba hili unapaswa kubadilishwa haraka kwa kushirikisha
vikao na kufuata taratibu zote za kisheria ikiwemo kupitishwa na baraza
la madiwani ili wananchi waweze kunufaika na ardhi yao na sio watu
wachache wanaolipwa mamilioni ya fedha bila ya sababu za msingi’’alisema
Gambo.
Naye
Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mhe. Julius Kalanga na Mwenyekiti wa
Halmashauri hiyo Mhe. Isack Joseph wote kwa pamoja waliunga mkono wazo
la Mkuu wa Mkoa na kusema kuwa watatoa ushirikiano wa dhati kuhakikisha
umiliki wa shamba hilo unabadilishwa na kwenda kwa vijiji hivyo.
Mkurugenzi wa TLCT Ndg. Boniface Ngimojiro akielezea muundo wa Taasisi hiyo yenye umiliki wa Shamba la Manyara Ranch.
Mkurugenzi
wa TLCT Bonfance Ngimojiro alipopewa nafasi ya kujieleza katika
mikutano hiyo miwili alisema kuwa taasisi hiyo inaongozwa na bodi ya
wadhamini yenye wajumbe nane wakiongozwa na Mbunge wa zamani wa Mondul,
Mhe. Edward Lowassa kama mwenyekiti wa Bodi hiyo.
Ngimonjiro
alikiri kupata amri ya kubadilishwa umiliki wa shamba hilo kutoka
katika taasisi hiyo kwenda kwa wananchi wa vijiji hivyo viwili lakini
yeye hawezi kujuwa ni kwa nini amri hiyo hadi jana haikutekelezwa.
Mkurugenzi
huyo alisema yeye ni mwajiriwa tu ambaye hajalipwa mishahara kwa miaka
zaidi ya minne sasa katika taasisi hiyo hivyo hawezi kujuwa kwa undani
zaidi kushindikana kutekelezwa kwa amri hiyo kwani wakitafutwa wahusika
wanaweza kuwa na majibu sahihi.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akikagua Boma la Ngombe lililopo katika shamba la Manyara Ranch.
Naye
Meneja wa AWF, Fidelis Ole Kashe yeye alisema kuwa wamekuwa wakifanya
kazi katika mazingira magumu sana ndani ya shamba hilo pamoja na
kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo katika shamba hilo ikiwemo
shule,zahanati ,ufugaji wa kisasa na machinjio.
Kashe
alisema utulivu ndio njia pekee itayofanya miradi iliyopo katika shamba
hilo kuendelea vinginevyo wafadhili hao wanaweza kusikitisha kila kitu.
Alisema
AWF imekuwa mstari wa mbele kufadhili miradi mbalimbali katika wilaya
ya Monduli na nchini kwa ujumla na inapenda kuona fedha inazotoa
zinafanya kazi iliyokusudiwa na sio vinginevyo.
Mbunge wa LongIDO Mhe. Julius Kalanga(kulia) akiwa na viongozi wa Chama cha Mapinduzi katika ziara ya Mkuu wa Mkoa.
Eneo la malisho kwa ajili ya Ngombe 780 waliopo katika shamba hilo na Kondoo 300.
SHARE
No comments:
Post a Comment