Mhe Ummy
akiongoza kikao cha Mawaziri wa Afya wa Afrika Mashariki. Kulia kwake ni
Mhe Christophe Bazivamo Naibu Katibu Mkuu wa EAC…na kulia ni Dr Kwessi
akimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Tanzania
NA MWANDISHI WETU – NAIROBI
Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
ameongoza kikao cha mkutano wa 13 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa
Afya wa nchi za Afrika Mashariki.
Mkutano huo ulifanyika juzi jijini Nairobi, Kenya ambapo pia ulijadili masuala mbalimbali yahusuyo sekta ya afya kwa ujumla.
Katika
taarifa yake aliyoituma kwa vyombo vya habari, Waziri Ummy alisema
mkutano huo ulihudhuriwa na Mawaziri wa Afya wa Kenya, Burundi, Uganda
pamoja na Mwakilishi wa Waziri wa Afya wa Rwanda.
“Mkutano huo ulitanguliwa na kikao cha wataalam na kikao cha makatibu wakuu wa wizara za afya katika nchi wanachama vilifanyika kuanzia Novemba 14 hadi 17, mwaka huu,” alisema.
“Mkutano huo ulitanguliwa na kikao cha wataalam na kikao cha makatibu wakuu wa wizara za afya katika nchi wanachama vilifanyika kuanzia Novemba 14 hadi 17, mwaka huu,” alisema.
Alisema
mambo makubwa yaliyojadiliwa na kupitishwa katika mkutano huo ni Sera ya
Afya ya EAC (EAC Regional Health Policy) na Sera, Mwongozo na Mkakati
wa EAC wa Afya ya Mama, Mtoto na Vijana (Intergrated EAC Reproductive,
Maternal, Newborn, Child and Adolescent Health Policy Guidelines and
Strategic Plan). “Sera hizi zitasimamia utekelezaji wa mipango ya
kuboresha na kuimarisha afya katika nchi wanachama wa Jumuiya kwa
utaratibu unaofanana,” alisema.
Waziri
Ummy alisema mkutano huo wa Mawaziri pia ulichambua na kupitia taarifa
ya Makatibu Wakuu wa Wizara za Afya ambapo ulieleza kuridhishwa na hatua
iliyofikiwa katika utekelezaji wa maagizo ya mawaziri wa afya ikiwemo
kuanzishwa kwa mpango wa pamoja wa kusimamia dawa, mpango wa pamoja wa
kukagua Vyuo Vikuu vya Afya pamoja na mpango wa pamoja wa huduma za
UKIMWI/VVU.
“Taarifa
ya Ukaguzi wa Vyuo Vikuu vya Afya vya Tanzania itawasilishwa katika
Kikao cha 14 cha Mawaziri wa Afya wa EAC kitakachofanyika Bujumbura
Machi, mwakani,” alisema. Aliwashukuru Mawaziri wa Afya wa Afrika
Mashariki kwa kuendelea kusimamia vyema utekelezaji wa sera na mipango
ya kuboresha na kuimarisha huduma za afya ktk nchi zao.
Aliwataka
kutekeleza maamuzi waliyokubaliana katika Mkutano huu ili kutimiza kwa
vitendo matarajio ya wananchi wa Afrika Mashariki ya kuwa na Afya bora.
Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Afya la EAC hufanyika mara
mbili kwa mwaka.
Lengo la
Mkutano huu ni kujadili utekelezaji wa sera, mipango na mikakati
mbalimbali ya kuboresha huduma za afya kwa nchi za Afrika Mashariki.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment