Wananchi
wa Mali wamepiga kura Jumapili hii Novemba 20 kwa uchaguzi wa mikoa,
hatua ya kwanza tangu uchaguzi wa rais Ibrahim Boubacar Keïta mwaka
2013, pamoja na kiwango cha ushiriki ambacho kimetangazwa kuwa cha chini
kabisa, kwa sababu ya kukosekana kwa utulivu katika nchi hii iliyo
chini ya hali ya dharura.
Uchaguzi
huu, ambao kiwancgo cha ushiriki kilikua hakijajulikana hadi saa sita
mchana umefanyika sanjari na maadhimisho ya kwanza ya mashambulizi ya
wanajihadi dhidi ya hoteli Radisson Blu mjini Bamako, ambapo watu 20
waliuawa, ikiwa nin pamoja na washambuliaji wawili.
"Uchaguzi
huu uliahirishwa mara nne. Hiyo inatosha, "amesema rais Keita baada ya
kupiga kura, huku akipongeza 'zoezi la kidemokrasia. '
Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon siku ya Jumamosi alitoa wito kwa
serikali, upinzani na makundi yaliyosaini mkataba wa amani wa mwezi Mei
hadi Juni 2015 "kuhakikisha uchaguzi unafanyika, bila vurugu, ambapo
hali ya kisiasa na usalama imekua ikiruhusu kufanyika kwa uchaguzi huo. "
Kwa
kutambua kuwa 'ucheleweshaji mkubwa katika utekelezaji wa masharti
muhimu ya mkataba', ikiwa ni pamoja na uanzishwaji wa mamlaka ya muda
katika eneo la Kaskazini, na 'hali ya usalama katika eneo la kaskazini
na baadhi ya maeneo ya kati mwa nchi vinaweza kuhatarisha maandalizi ya
uchaguzi ', Ban Ki-moon alitoa wito kwa serikali" kupunguza mvutano
"ambao unaweza kusababisha hali hiyo.
Chanzo cha utawala kimebaini kwamba hali ya sintofahamu imeripotiwa katika mji mkuu wa nchi hii, Bamako na katikati mwa nchi.
Zoezi la kupiga kura halikufanyika katikajimbo la Kidal, kaskazini-mashariki mwa nchi, ngome ya kundi la waasi la Azawad.
Katika jimbo jirani la Gao, uchaguzi umefanyika katika baadhi ya wilaya.
Katika
jimbo la Timbuktu, kaskazini-magharibi mwa nchi, ambapo vifaa vya
uchaguzi viliondolewa na kuchomwa moto wakati mashambulizi tofauti,
ikiwa ni pamoja na Jumapili. Kama uchaguzi ulifanyaka kwa hali ya
utulivu katika mji wa jimbo hilo, katika maeneo mengine kuliripotiwa
vurugu na pia haukufanyika katika baadhi ya maeneo ya jimbo hilo.
"Watu
hawakujitokeza kwa wingi. Kulikuwa na wasiwasi, lakini wote hali ni
nzuri mpaka sasa, "Oumar Moussa capita Sareykeyna, mtuu maarufu katika
jimbo la Timbuktu, ameliambia shirika la habari la AFP.
Itafahamika
kwamba mgombea wa chama kidogo cha upinzani alitekwa nyara siku ya
Jumamosi asubuhi katika eneo la Koro, katikati mwa nchi, amesema
kiongozi wa chama cha mgombea huyo, Mamadou Sidibé, akiongeza kuwa "gari
la Saibou Barry lilichomwa moto na yeye mwenyewe alipelekwa katika eneo
lisilojulikana. " RFI
SHARE
No comments:
Post a Comment