Mmoja wa
Wakufunzi wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) akimwonyesha Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani, moja ya
vifaa vinavyotumiwa na abiria wakati meli inapozama wakati Naibu Waziri
huyo alipohudhuria mahafali ya 12 ya chuo hicho, jijini Dar es Salaam.
Mhandisi
wa Meli kutoka Chuo cha Bahari Dar es Salaam, Capt. Jumanne Karume.
akimwelezea Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin
Ngonyani namna meli inavyoendeshwa kwenye chumba cha nahodha,
alipotembelea chuo hicho wakati wa mahafali ya 12 ya chuo hicho jijini
Dar es Salaam.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani
(kushoto), akiwatunuku wahitimu wa moja ya kozi zinazotolewa na Chuo cha
Bahari Dar es Salaam (DMI), jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani (kulia),
akimkabidhi zawadi mwanafunzi aliyefanya vizuri katika mahafali ya Chuo
cha Bahari Dar es Salaam (DMI), jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani (kulia)
na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya DMI, Bi. Rukia Shamte, wakiangalia
zawadi aliyopewa mgeni rasmi na Chuo hicho katika mahafali ya chuo
hicho, jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani,
ameutaka uongozi wa Chuo cha Bahari cha Dar es salaam (DMI), kubuni na
kutafuta vyanzo madhubuti vya mapato ili kusaidia kutatua changamoto
zilizopo chuoni hapo.
Akizungumza
katika Mahafali ya 12 ya Chuo hicho yaliyofanyika jijini Dar es salaam,
Mhandisi Ngonyani amesema kuwa uwepo wa vyanzo imara vya mapato chuoni
hapo utapelekea kutimiza malengo yake ya kutoa elimu na mafunzo
yanayokubalika ndani na nje ya nchi.
“Wizara
ingependa kuona DMI inaongeza ubunifu wa kutafuta vyanzo madhubuti vya
mapato, Mkiwa na fedha mtaweza kutatua changamoto ndogo ndogo mlizonazo
na kufikia malengo mliojiwekea”, amesema Mhandisi Ngonyani.
Ameutaka
uongozi huo kukamilisha na kuwasilisha haraka upembuzi yakinifu na
usanifu wa kina wa mahitaji halisi ya majengo ya madarasa na ofisi za
walimu ili kuiwezesha serikali kuchukua hatua stahiki.
Aidha,
amewahakikishia wanafunzi kuwa Serikali itaendelea kusimamia mazoezi ya
vitendo kwa wanafunzi wanaochukua fani mbalimbali chuoni hapo ili waweze
kukubalika ndani na nje ya nchi.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Bodi chuoni hapo Bi Rukia Shamte,
amemhakikishia Naibu Waziri huyo kukamilisha taarifa ya Upembuzi
yakinifu na kuiwasilisha kwake ili kuweza kufanyiwa kazi.
Ameiomba
Serikali kuongeza bajeti kwa ajili ya chuo hicho ili kuboresha
miundombinu ya chuo ikiwemo ununuzi wa vifaa mbalimbali vya mafunzo na
ujenzi wa madarasa.
“ Kwa
sasa tupo katika hatua ya mwisho za kumaliza upembuzi yakinifu na
usanifu wa kina wa ujenzi wa jengo la wakufunzi pamoja na madarasa ili
kukifanya chuo kibaki kwenye hadhi ya kimataifa, tukimaliza
tutawasilisha serikalini kwa hatua zaidi, amesema Mwenyekiti wa Bodi
Zaidi ya wahitimu 70 wa fani mbalimbali wamehitimu katika mahafali ya 12 ya chuo hicho yaliyofanyika jijini Dar es salaam.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.(P.T)
Na.Alex Mathias.
Kampuni ya
Hawai Product imeingia makubaliano na timu ya Mbao Fc kwa ajili ya
udhamini wa timu hiyo, mkataba wenye thamani ya shilingi milioni 25 kwa
mzunguko wa pili pekee.
Akiongea
mbele ya waandishi wa Habari leo hii,meneja wa masoko wa kampuni hiyo
inayoratibu maziwa ya cowbel Elisharia Ndeka amesema kwamba wameamua
kutoa udhamini kwa klabu hiyo baada ya kurizishwa na kiwango chao katika
ushiriki wa michezo ya ligi kuu ya Tanzania bara.
Nae
mwenyekiti wa Mbao FC ya Ilemela jijini Mwanza Solly Zephania
ameishukuru kampuni hiyo kwa kufanikisha udhamini huo kwani kwa mujibu
wa taarifa yake utakuwa na tija kwao hasa katika maswala ya uendeshaji
wa timu.
Amesema
kwamba udhamini huo wa shilingi milioni 25 unaweza kuongeza mara baada
ya miezi sita kumalizika endapo timu hiyo itaendelea kufanya vizuri
kwenye michezo ya ligi kuu ya Tanzania bara.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment