Mwakilishi
wa Mkuu wa Mkoa wa Singida Bw. Buhacha Baltazar Kichinda ambaye ni
Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya utawala na rasilimali watu akiwaaga
Vijana 43 wanaojiunga na kambi ya JKT Makutopora kikosi cha KJ 834 kwa
hiyari kwa mkataba wa miaka ya miwili. Bw. Kichinda amesema wakiwa
jeshini watafundishwa uzalendo, ukakamavu, stadi za jamii na nidhamu,
amewaasa wazazi kuwapeleka shule wanafunzi na kupokea fursa kama za
jeshi.
Afisa
Tawala ofisi ya Mshauri wa Mgambo Rhinocerus Magembesoni akiwaasa vijana
43 wa kihadzabe wakipanda mabasi kuelekea katika kambi ya JKT
Makutopora kikosi cha KJ 834 kujiunga na kikosi hicho kwa hiyari kwa
mkataba wa miaka ya miwili mara baada ya kuagwa na mwakilishi wa Mkuu wa
Mkoa wa Singida. Jamii ya kihadzabe huendesha maisha yao kwa kuwinda na
kula nyama pori, matunda ya porini, asali na mizizi.
Vijana 43
wa kihadzabe wakipanda mabasi kuelekea katika kambi ya JKT Makutopora
kikosi cha KJ 834 kujiunga na kikosi hicho kwa hiyari kwa mkataba wa
miaka ya miwili mara baada ya kuagwa na mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa
Singida. Jamii ya kihadzabe huendesha maisha yao kwa kuwinda na kula
nyama pori, matunda ya porini, asali na mizizi.
Mmoja wa
kijana wa kihadzabe Zuhura Ramadhani Longa ambaye alikuwa akiwasindikiza
vijana wenzake wanawinda na kurina asali, amesema ameamua kujiunga na
jeshi ili aweze kuisaidia familia yake lakini pia aweze kulitumikia
taifa.
Vijana 43
wa kihadzabe wakipunga mikono kuonyesha utayari wa kujiunga na kambi ya
JKT Makutopora kikosi cha KJ 834 kwa hiyari kwa mkataba wa miaka ya
miwili mara baada ya kuagwa na mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Singida.
Jamii ya kihadzabe huendesha maisha yao kwa kuwinda na kula nyama pori,
matunda ya porini, asali na mizizi.
Vijana wa
kihadzabe ambao walikuwa wanawinda na kurina asali, wamesema wameamua
kujiunga na jeshi ili waweze kusaidia familia yake lakini pia waweze
kulitumikia taifa.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment