Katibu
Tawala mkoa wa Mara, Adoh Mapunda (katikati) akizungumza hii leo kwenye
kilele cha mafunzo ya siku tatu kwa wadau wa filamu mkoani humo. Mafunzo
hayo yalianza juzi Disemba 14,2016 kwenye ukumbi wa shule ya Sekondari
Mara Mjini Msoma.
Yaliandaliwa
na Bodi ya Filamu nchini kwa lengo la kuwajengea welezi wanatasinia wa
filamu ili kuzalisha kazi zenye ubora na hivyo kukidhi ushindani katika
soko la ndani na nje ya nchi ambapo zaidi ya washiri 200 walionufaika na
mafunzo hayo wamepatiwa vyeti. Tayari mafunzo ya aina hiyo yamefanyika
mikoa ya Morogoro na Mwanza na yataendelea katika mikoa mingine. BMGHabari
Wanatasnia
wa filamu mkoani Mara wakimsikiliza Katibu Tawala mkoani humo, Adoh
Mapunda, wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa wanatasnia hao.
Ameahidi kutoa fulana (Tshirt) 250 kwa ajili ya wanatasnia wa filamu
mkoani Mara waliohudhuria mafunzo hayo ambapo zitawasaidia hususani kuwa
na sare ya aina moja wakikutana kwa pamoja
Naibu
Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi.Nuru
Millao, amesema sekta ya filamu ina mchango mkubwa katika kukuza uchumi
wa wanatasnia wake na taifa kwa ujumla hivyo Bodi za filamu mikoani
zihakikishe zinasimamia maendeleo ya tasnia hiyo.
Katibu
Mtendaji Bodi ya Filamu nchini, Bi.Joyce Fisso, amebainisha kwamba wadau
wa filamu wakiwemo watayarishaji, waongozaji, wahariri pamoja na
waigizaji wamefundishwa vyema mafunzo hayo ili kuzalisha kazi bora.
Mgeni
rasmi, Katibu Tawala mkoani Mara, Adoh Mapunda (wa pili kulia), akipokea
cheti cha utambuzi kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi.Nuru Millao
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi.Nuru Millao, akipokea cheti cha utambuzi.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment