Wachezaji
wa timu za Bandari ya Dar es Salaam na Makao Makuu wakichuana kwenye
mchezo wa mpira wa kikapu uliochezwa kwenye uwanja wa Bandari Tanga
ambao ulimalizika kwa Bandari Dar kuibuka na ushindi wa vikapu 50 -47
Wachezaji
wa timu za Bandari ya Dar es Salaam na Makao Makuu wakichuana kwenye
mchezo wa mpira wa kikapu uliochezwa kwenye uwanja wa Bandari Tanga
ambao ulimalizika kwa Bandari Dar kuibuka na ushindi wa vikapu 50 -47
Wachezaji
wa kuvuta kamba timu ya Bandari ya Tanga wakichuana dhidi ya Makao
Makuu mchezo umalizika kwa Tanga kuibuka na ushindi wa seti 2-0 mchezo
uliochezwa viwanja vya Shule ya Sekondari Popatlaly mjini Tanga
TIMU
ya Mpira wa Pete ya Bandari ya Tanga leo wameweza kuibuka na ushindi wa
mabao 43-16 dhidi ya Bandari ya Mtwara kwenye michuano ya Bandari
inayoendelea mjini Tanga.
Mchezo
huo ambao ulichezwa kwenye viwanja vya Bandari mjini hapa ambapo mpaka
timu zote zinakwenda mapumziko Bandari Tanga ilikuwa ikiongozwa kwa
mabao 23 -17 dhidi ya Mtwara.
Halikadhalika
Tanga wakiweza kuibuka pia na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Makao Makuu
kwenye mchezo wa mpira wa miguu uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya
sekondari Popatlaly mjini hapa.
Katika
mchezo mwengine uliochezwa kwenye uwanja huo timu ya Bandari ya Dar es
Salaam iliweza kuibuka na ushindi dhidi ya Makao Makuu kwa mabao 36-13.
Wakati
huo huo,Timu ya Bandari ya Dar es Salaam imeweza kuibuka na ushindi wa
vikapu 50 -47 dhidi ya Makao Makuu kwenye mchezo wa mpira wa kikapu
uliochezwa kwenye dimba hilo la Bandari mjini hapa.
Kwenye
mchezo mpira wa miguu uliozikutanisha Bandari Mtwara na Maziwa Makuu
ambapo timu hizo mpaka dakika 90 zilijikuta zikigawana pointi moja moja
baada ya kutoka sare ya kufungana bao 1-1.
Ili
kuonyesha wana umahiri mkubwa kwenye michezo Bandari Tanga wanaume
waliweza kuibuka na ushindi wa seti 2-0 dhidi ya Makao Makuu kwenye
mchezo wa kuvuta kamba.
Wakati
wanaume wakiibuka na ushindi huo wanawake nao waliweza kuwaunga mkono
wenzao kwa kuibuka na ushindi wa seti 2-0 dhidi ya Makao makuu kwenye
mchezo wa kuvuta kamba uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya Sekondari
Popatlaly.
Mashindano
hayo ambayo yalifunguliwa jana na Mkurugenzi wa Bandari nchini (TPA)
Deusdedit Kakoko ambaye aliwataka wanamichezo hao kuzingatia nidhamu na
maarifa kwenye michezo yao ili kupata ushindi.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment