Na Hassan Mabuye (Kitengo cha Mawasiliano - Wizara ya Ardhi)
Waziri
wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amekutana
wakazi wa Shinyanga na kusikiliza kero zao za ardhi na kuzitatua ambapo
wananchi walijitoka kwa wingi katika viwanja vya Zimamoto Nguzo Nane
mjini Shinyanga ambapo Waziri Lukuvi
amepokea kero zaidi ya 200 za ardhi mkoani Shinyanga zinazodaiwa
kuchangiwa kwa kiasi kikubwa na maafisa ardhi,wenyeviti wa mitaa
waliojikuta wakishindwa kujibu kero hizo mbele ya waziri huyo.
Waziri
Lukuvi alisema baada ya kupokea kero hizo ataunda kikosi maalum cha
wataalam watakaoweka kambi mkoani Shinyanga kwa ajili ya kusikiliza kero
za wananchi na wataitwa mmoja mmoja kisha kujibiwa kwa maandishi.
“Kama
mmekaa na kero za ardhi tangu mwaka 2008 mpaka leo,naomba mniamini basi
mimi kwa sababu Waziri ndiyo mwenye majibu ya mwisho kuhusu kero
zenu,nilichobaini viongozi hawasikilizi kero za wananchi, kuna kero
zingine hazikupaswa kuletwa kwangu mngemalizana huko huko”,alieleza
Waziri Lukuvi.
“Kama
kuna maafisa ardhi wamekuwa sehemu ya migogoro ya ardhi lazima
wawajibishwe,haiwezekani wananchi waichukie serikali kwa sababu ya
watendaji wasio waaminifu,kiongozi atayebainika kuigombanisha serikali
na wananchi tutaachana naye”,aliongeza Lukuvi.
Waziri
Lukuvi ametoa wito kwa wananchi wenye kero za ardhi wanapotoa ushahidi
wawataje kwa majina watu wote waliohusika katika kukuza migogoro ya
ardhi na kusababisha wananchi kunung’unika kwa kukosa haki zao ili
waweze kuchukuliwa hatua.
Kufuatia
udhaifu huo aliwataka viongozi akiwemo Mkuu wa Mkoa na Wakuu wa Wilaya
na Wakurugenzi wa Halmashauri kupanga muda wa kusikiliza kero za
wananchi ili kupunguza kero za wananchi.
Wakizungumza
mbele ya waziri huyo,wananchi walisema baadhi ya watendaji wa
serikali,wenyeviti wa mitaa na maafisa ardhi wamekuwa chanzo kikubwa cha
migogoro kwa kuendekeza rushwa na kujuana.
Mheshimiwa
William Lukuvi akiwa wilani kishapu Mkoani Shinyanga ameendelea na
ziara ya kusikiliza kero za wananchi kuhusu masuala ya ardhi na
kuzitatua.
Akizungumza
katika viwanja vya Ushirika katika mji wa Mhunze wilayani Kishapu wenye
kata 25,vijiji 117 na vitongoji 660 wakati akisikiliza kero za ardhi
kutoka kwa mwananchi mmoja baada ya mwingine,Waziri Lukuvi alisema
Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli
imedhamiria kumaliza kero za ardhi.
Ziara
hiyo imekuwa na manufaa kwa wakazi wa Kishapu baada ya waziri huyo
kuahidi kuanzisha baraza la ardhi katika wilaya hiyo hivi karibuni na
wiki ijayo atateua mwenyekiti wa Baraza hilo ili kutatua kero za ardhi
na kuwapunguzia wananchi adha ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma
hiyo katika wilaya ya Shinyanga.
Lukuvi
aliwataka maafisa wa ardhi nchini kushirikiana na sekta binafsi kupanga
miji na wao kubakia kuwa wasimamizi wa taratibu zote kwani serikali
haina uwezo wa kuajiri maafisa ardhi na mipango miji wengi.
Waziri
Lukuvi pia amepiga marufuku vitendo vinavyofanywa na baadhi ya
wawekezaji wasio waaminifu waliopewa vibali vya kuchimba madini
kuwahamisha wananchi katika maeneo ya uchimbaji bila kuwalipa fidia.
“Kama
umepewa kibali na serikali cha kuendeleza eneo flani la mgodi wale
wananchi wa pale lazima waondoke lakini waondolewe kwa heshima, wapewe
fidia inayofanana na thamani ya mali zao zilizopo eneo lenye mgodi siyo
fidia ya kupunza wananchi kama kulikuwa kuna nyumba wajengee nyumba
zingine nzuri ndio uwaamishe”,alisema Lukuvi.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi
akisalimiana na Maafisa wa Serikali mkoani Shinyanga mara baada ya
kuwasili katika wilaya hiyo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga
Josephine Matiro.
Wananchi
wa Mkoa wa Shinyanga wakiwa katika foleni ya kukabidhi malalamiko yao
ya migogoro ya ardhi na bahasha za kero za ardhi kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi ili atolee ufumbuzi.
Bahasha
zaidi ya mia mbili (200) za kero za migogoro ya ardhi zikiwa
zimepokelewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.
William Lukuvi ili aitatue.
Wananchi wa Mkoa wa Shinyanga wakiandaa maelezo kuhusu matatizo wanayokumbana nayo katika umiliki wa ardhi mkoani Shinyanga ili Waziri wa Ardhi ayatatue.
Wananchi wa Mkoa wa Shinyanga wakiwa eneo la mkutano wakisubiri zamu ya kueleza kero za ardhi kwa waziri.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akitatua
mgogoro wa ardhi wa Bibi Safina Ibrahim mara baada ya kuleta vielelezo
vyake.
Msafara
wa Waziri wa Ardhi, ukiwa umewasili katika jengo la Halmashauri ya
wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga kwa ajili ya kukutana na wakuu wa
idara hususani wa sekta ya ardhi wa Kishapu kabla ya kwenda katika
mkutano wa kusikiliza kero za wananchi katika mji wa Mhunze.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimkabidhi
vitabu vyenye muongozo namna ya kupanga miji sambamba na kitabu chenye
majina 33 ya makampuni yaliyojitolea kushirikiana na serikali kupima
ardhi.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akitatua
mgogoro wa ardhi wa wananchi wa Kishapu waliokuwa wanagombea eneo la
makazi.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimhoji
Mthamini wa wilaya ya Kishapu Reuben Lauwo (mwenye shati ya bluu) na
Afisa Ardhi wa wilaya ya Kishapu Grace Pius (gauni la kitenge) kwanini
hawakumlipa fidia bwana Daudi Amos (wa kwanza kushoto) kama
inavyostahiki.
SHARE
No comments:
Post a Comment