Waziri
Mkuu wa Italia, Matteo Renzi amesema atajiuzulu, baada ya kushindwa
katika kura ya maoni iliyofanyika jana Jumapili, kuhusu mapendekezo yake
ya kuifanyika mageuzi katiba ya nchi hiyo.
Akilihutubia
taifa kupitia televisheni baada ya matokeo ya awali kutangazwa, Renzi
amesema majukumu ya serikali yake yamemalizika leo. Matokeo hayo
yanaonyesha kambi yake ya kura ya 'Ndiyo' imeshindwa katika uchaguzi huo
kwa kupata kati ya asilimia 42 na 46. Kambi ya 'Hapana' imepata kati ya
asilimia 54 na 58 ya kura.
Renzi
amesema leo mchana ataitisha kikao na baraza lake la mawaziri na kisha
atawasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa Rais Sergio Mattarella.DW
SHARE
No comments:
Post a Comment