Rais wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amewapongeza
viongozi wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), waliochaguliwa kushika
nyadhifa mbalimbali katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwishoni mwa wiki
iliyopita.
Katika
salamu zake za kuwapongeza viongozi hao, Rais Malinzi amesema huu ni
wakati mwafaka wa kujipanga katika kufuzu michuano ya kimataifa
tukianzia hii Olimpiki ya mwaka 2020 itakayofanyika Tokyo, Japan.
Kuonyesha
namna TFF ilivyopjipanga kwa ajili ya maandalizi hayo, msimu huu
imeendesha Ligi Kuu ya Soka Taifa kwa upande wa wanawake na wavulana
wenye umri wa chini ya miaka 23, lengo likiwa ni kupata timu ya kutafuta
kufuzu.
Tumewaomba
wanafamilia wa mpira wa miguu kupendekeza majina majina ya timu za
taifa za wanawake na wavulana wenye umri wa chini ya miaka 23 kabla ya
timu hizo hazijaingia kwenye kalenda ya kutafuta timu za kufuzu kwa
kushirikiana na TOC.
Kwa
Malengo yote hayo na mengine, TFF inaahidi kushirikiana na TOC na vyama
vingine vya michezo kikiwamo cha riadha ambacho pia kimepata viongozi
wake hivi karibuni.
TFF
inaamini itapata ushirikiano wa kutosha kutoka timu nzima ya Viongozi wa
TOC watakaoongoza kwa miaka minne ijayo, kuanzia sasa hadi kipindi cha
Olimpiki ya Tokyo 2020 ambao ni Rais Gulam Rashid aliyepata kura za
ndiyo 48 na mbili za hapana na Makamu wa Rais, Henry Tandau aliyepata
kura za ndiyo 44, tano zikimkataa na moja ikiharibika.
Wengine
ni Katibu Mkuu, Filbert Bayi aliyetetea kwa kishindo nafasi yake hiyo
baada ya kupata kura za ndiyo 49, huku hapana moja huku Katibu Msaidizi
Suleiman Mohamed Jabir akichomoza kwa kura 49 huku moja ikimkataa na
Mweka Hazina ni Charles Nyange kura za ndiyo 47 huku hapana ni tatu na
Mweka Hazina Msaidizi alichaguliwa Juma Khamis Zaidy kura 47, moja
ikiharibika na hapana ni mbili.
Katika
uchaguzi huo ulioendeshwa na kufanyika kwa utulivu mkubwa, Mwenyekiti wa
Kamisheni ya Uchaguzi, Wakili Lloyd Nchunga, aliwataja walioshinda
nafasi tano za Ujumbe wa Kamati ya Utendaji kutoka Bara na kura zao
kwenye mabano kuwa ni Irene Mwasanga (50), Noorelain Sharrif (48),
Muharam Mchume (39), Amina Lyamaiga (32), na Donath Massawe (30).
Kwa
upande wa Wajumbe wa Kamati ya Utendaji Zanzibar walishinda ni Kocha wa
Timu ya Taifa ya Wanawake ‘Twiga Stars’, Nasra Juma Mohamed (44), Katibu
wa Chama cha Riadha Zanzibar (ZAAA), Suleiman Ame Khamis (42), Mussa
Abdulrabi Fadhi (37), Ramadhan Zimbwe Omar (33), na Sheha Mohammed Ali
(30).
Kwa
upande wa Wana Olimpiki, Mwanariadha wa kike, Zakia Mrisho alishinda kwa
kura 49, Samuel Mwera kura 48 na Fabian Joseph kura 44. Nafasi za juu
ambazo zilikuwa na mgombea mmoja mmoja.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment