Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine
Mahiga kwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Mhe. Balozi Dkt.
Amina Mohammed wakisaini Makubaliano ya Tume ya Pamoja ya Ushirikiano
kati ya Tanzania na Kenya. Makubaliano hayo yamesainiwa kufuatia Kikao
cha Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (JCC) kati ya Tanzania na Kenya
kilichofanyika tarehe 1 hadi 3 Desemba, 2016 ambapo masuala mbalimbali
ya ushirikiano baina ya nchi hizi mbili yalijadiliwa na kukubaliwa.
Masuala ya ushirikiano ni pamoja na kilimo, uchukuzi, utalii, nishati na
madini na uvuvi. Hafla hiyo fupi ya uwekaji saini makubaliano hayo
imefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere
Jijini Dar es Salaam tarehe 16 Desemba, 2016.
Waziri Mahiga na Waziri Mohammed wakibadilishana makubaliano hayo mara baada ya kusaini.
Waziri
Mahiga akizungumza katika hafla hiyo.Katika hotuba yake Mhe. Mahiga
alisisitiza kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana kwa karibu na Kenya na
kwamba makubaliano yaliyosainiwa yataimarisha mahusiano hayo kwa
kuboresha mazingira ya uwekezaji, kurahisisha ufanyaji biashara na
kuongeza fursa za ajira kwa vijana wa nchi hizi mbili.
Waziri
Amina naye akizungumza kwenye hafla hiyo. Katika hotuba yake aliahidi
Kenya kuendelea kushirikiana na Tanzania kwa karibu katika masuala yote
yaliyokubaliwa.
Kaimu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi akitoa neno la shukrani
katika hafla hiyo ya uwekaji saini Makubaliano ya Tume ya Pamoja ya
Ushirikiano
Sehemu ya
wajumbe kutoka Kenya waliohudhuria hafla ya uwekwaji saini wa
Makubaliano ya Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya.
Kulia ni Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Chirau Ali Mwakwere
Sehemu ya
ujumbe wa Tanzania nao wakishuhudia uwekwaji saini katika makubaliano
ya tume ya pamoja ya ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya. Kushoto ni
Balozi Samwel Shelukindo, Mkurugenzi wa Idara ya Afrika akifuatiwa na
Bw. Stephen Mbundi, Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama
katika Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masahriki
Mshereheshaji
ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano katika Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga akiwakaribisha
wageni wakati wa hafla ya uwekaji saini Makubaliano ya Tume ya Pamoja
ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya.
Sehemu ya maafisa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Waandishi wa Habari waliohudhuria hafla hiyo.
Picha ya Pamoja(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment