Duru la
Pili la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuanza leo
Jumamosi Desemba 17 kwa michezo minne kabla ya michezo mingine minne
kufanyika siku ya Jumapili Desemba 18, mwaka huu.
Katika
mechi za Leo, Mabingwa watetezi wa taji hilo, Young Africans SC ya Dar
es Salaam itakuwa mgeni wa JKT Ruvu ya Pwani kwenye mchezo utakaofanyika
Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Licha ya
kwamba mwenyeji wa mchezo huo ni JKT Ruvu ambayo uwanja wake wa nyumbani
mara nyingi huwa ni Mabatini ulioko Mlandizi, lakini kwa mujibu wa
Kanuni ya 6 (5) na (6) ya Ligi Kuu Bara, mechi zake za nyumbani dhidi ya
Simba, Young Africans na Azam FC, hufanyika Uwanja wa Uhuru.
Michezo
mingine ya leo ni Kagera Sugar kuwa mgeni wa Mbeya City kwenye Uwanja wa
Sokoine jijini Mbeya wakati Ruvu Shooting ya Pwani itakuwa mwenyeji wa
Mtibwa Sugar ya Morogoro kwenye Uwanja wa Mabatini, Pwani ilihali Mwadui
ya Shinyanga itaikaribisha Toto Africans ya Mwanza kwenye Uwanja wa
Mwadui Complex.
Jumapili,
Desemba 18, mwaka huu Mbao FC ya Mwanza itacheza na Stand United ya
Shinyanga kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza wakati Ndanda itakuwa
mwenyeji wa Vinara wa Msimamo katika Ligi Kuu ya Vodacom, Simba kwenye
Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.
African
Lyon ya Dar es Salaam itaikaribisha Azam FC pia ya Dar es Salaam kwenye
Uwanja wa Uhuru jijijini siku hiyo ya Jumapili wakati Majimaji ya Songea
itakuwa Mbeya kucheza na Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, limetoa masharti kadhaa likitaka klabu za Ligi Kuu ya Vodacom kufuata.
Masharti
hayo, ni kwa klabu kutumia makocha wenye sifa kwa mujibu wa kanuni ya 72
ya Ligi Kuu ya Vodacom. Kwa mujibu wa Bodi ya Ligi Kuu ya Shirikisho la
Mpira wa Tanzania (TFF) na kwa mujibu wa kanuni hiyo, makocha
wanaopaswa kukaa kwenye benchi la Ligi kuu kwa msimu huu wasipungue sifa
ya kuwa na leseni B ya CAF.
Pia kwa
timu za Ligi Daraja la Kwanza na Pili, masharti ni lazima makocha wawe
na sifa za kuzinoa timu hizo ambazo zimeanishwa kwenye kanuni za ligi
husika.
Kadhalika,
tunaagiza klabu kutotumia wachezaji wa kigeni au makocha kama hawana
vibali vya ukaazi na kufanya kazi kutoka Idara ya Uhamiaji nchini
iliyoko chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani. (P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment