TRA

TRA

Saturday, January 14, 2017

AU yatishia hatua kali dhidi ya Yahya Jammeh

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Rais Yahya Jammeh wa Gambia
Rais Yahya Jammeh wa Gambia
Muungano wa Afrika AU umesema kuwa utawacha kumtambua Yahya Jammeh kama rais wa Gabon kuanzia tarehe 19 Januari wakati muda wake utakapokamilika.
Baraza la amani na usalama la muungano huo pia limetishia kuchukua hatua kali iwapo vitendo vya Jammeh vitasababisha mauaji ya raia wasio na hatia.
Muungano huo pia umevitaka vikosi vyake vya kulinda amani kujizuia.
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari yuko nchini Gambia akiongoza ujumbe wa mataifa ya magharibi ECOWAS katika jaribio la hivi karibuni kumshawishi bwana Jammeh kuwachilia mamlaka kwa Adama Barrow ambaye alishinda uchaguzi wa urais mwezi uliopita.
Adama Barrow na Yahya Jammeh
Adama Barrow na Yahya Jammeh
Bwana Barrow ameambia BBC kwamba ataapishwa kama rais wiki ijayo na kumtaka Jammeh ashiriki katika mazungumzo na wapatanishi hao.
Aidha memtaka Rais anayemaliza muda wake Yahya Jammeh kushiriki katika mazungumzo ya moja kwa moja ili kutatua mgogoro wa kisiasa ulioikumba nchi hiyo.BBC

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger