Kiongozi wa baraza la Seneti nchini Nigeria amesema kwamba Rais
Muhammadu Buhari yuko katika hali nzuri kiafya mjini London, akijaribu
kutupilia mbali uvumi juu ya hali ya afya ya rais huyo. Bukola Saraki
alikwenda katika mji mkuu wa Uingereza pamoja na kiongozi wa wajumbe
walio wengi katika baraza la Seneti, Ahmed Lawan, na spika wa baraza la
wawakilishi, Yakub Dogora. Ni ujumbe wa hivi karibuni kabisa wa kisiasa
kumtembelea kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 74 katika makaazi rasmi
ya ubalozi wa Nigeria nchini Uingereza, ambako amekuwa akiishi kwa
karibu mwezi mmoja. Saraki amesema katika taarifa kwenye ukurasa wa
mtandao wa kijamii wa Facebook kwamba Buhari yuko katika hali nzuri
kiafya, na hakuna sababu ya wasiwasi. Katika ukurasa wa Twitter, Buhari
ameandika jana kwamba amefurahishwa na ziara hiyo na kuwashukuru
Wanigeria, Wakristo na Waislamu kwa dua zao na kumtakia kheri ya afya
njema.
Friday, February 17, 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment