Mwenyekiti
wa Mkutano wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya
kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya
maendeleo endelevu ambaye pia ni Mkurugenzi wa UNESCO Kanda ya Mashariki
mwa Afrika, Bi. Ann Therese Ndong-Jatta akiendesha mjadala wa
kuhitimisha mkutano huo wa siku mbili wa wadau wa elimu kutoka nchi 13
uliofanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere International Conventional
Centre (JNICC) jijini Dar es Salaam. (Habari picha na Zainul Mzige)
Mkurugenzi
Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller, iliyona
makazi yake nchini Marekani akielezea kuhusu mradi wa XPRIZE unahusisha
watoto ambao hawapo shuleni ukiwa na malengo ya kukuza teknolojia ya
dunia kwa kutumia uwezo walionao ukilenga watoto wa miaka 5-12 wakati wa
kuhitimisha mkutano wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna
ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia
ya maendeleo endelevu uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce
Ndalichako akielezea jitihada zitakazofanywa na serikali ya Tanzania
katika kuboresha sekta ya elimu kuelekea utekelezaji wa SDG4 kwenye
mkutano wa siku mbili wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna
ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia
ya maendeleo endelevu uliofanyika jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Elimu, Rasilimali Watu na Tafiti za Kisayansi wa Mauritius, Leela
Dookon Luchoomon (kushoto) akieleza mipango ya serikali yake katika
kuboresha elimu wakati wa kuhitimisha Mkutano wa mawaziri wa Afrika
Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4)
kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu uliofanyika jijini Dar
es Salaam na kuandaliwa na UNESCO kwa kushirikiana na ILO, UNFPA, UNDP,
UNICEF, UN Women, UNHCR pamoja na World Bank.
Balozi
wa Canada nchini Tanzania, Ian Myles akizungumza kwa niaba ya nchi
wahisani wakati wa kuhitimisha Mkutano wa mawaziri wa Afrika Mashariki
wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya
malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu
Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi wa Djibouti, Mh. Moustapha Mohamed
Mahamoud akiwasilisha mapendekezo ya serikali yake katika kuhitimisha
Mkutano wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha
lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo
endelevu uliofanyika jijini Da es Salaam.
Waziri
wa Elimu na shule za msingi wa Uganda, Mh. Nansubuga Rosemary Seninde
(kulia) akitoa mapendekezo ya serikali yake katika kuboresha elimu
kwenye mkutano wa siku mbili wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili
namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya
dunia ya maendeleo endelevu uliofanyika jijini Da es Salaam. Kushoto ni
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma.
Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Mh. Mhandisi
Stella Manyanya (kulia) na Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Leonard
Akwilapo wakiandika mapendekezo muhimu yaliyokuwa yakiwasilisha kwenye
mkutano wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha
lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo
endelevu uliofanyika jijini Da es Salaam.
Sehemu
ya mawazi wa elimu kutoka Kenya, Uganda, Sudan Kusini, Ethiopia,
Somalia, Comoro na Djibouti walioshiriki kwenye mkutano wa mawaziri wa
Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu
(SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu uliofanyika
jijini Da es Salaam.
Sehemu
ya wadau wa sekta ya elimu kutoka nchi 13 walioshiriki kwenye mkutano
wa siku mbili wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya
kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya
maendeleo endelevu uliofanyika jijini Da es Salaam.
Mwenyekiti
wa Mkutano wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya
kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya
maendeleo endelevu ambaye pia ni Mkurugenzi wa UNESCO Kanda ya Mashariki
mwa Afrika, Bi. Ann Therese Ndong-Jatta akifuatilia mijadala mbalimbali
iliyokuwa ikiwasilishwa na wadau wa sekta ya elimu wakati wa mkutano
huo uliofanyika jijini Da es Salaam.
Mkuu
wa Ofisi na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira
Rodrigues (katikati) akibadilishana mawazo na baadhi ya washiriki wa wa
mkutano wa siku mbili wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna
ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia
ya maendeleo endelevu uliofanyika jijini Da es Salaam.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) walioshiriki kufanikisha mkutano wa siku
mbili wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha
lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo
endelevu uliofanyika jijini Da es Salaam.
Afisa
mipango kutoka UNESCO, Bi Faith Shayo (kushoto) akijadiliana jambo na
wafanyakazi wenzake wakati wa mkutano wa siku mbili wa mawaziri wa
Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu
(SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu uliofanyika
jijini Da es Salaam.
Na Zainul Mzige
Waziri
wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce
Ndalichako amesema kwamba wizara yake itashirikiana na wizara nyingine
nchini kuhakikisha kwamba migogoro ya walimu inamalizwa ili kufanikisha
utoaji wa elimu kuwa bora na jumuishi.
Kauli
hiyo aliitoa wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari katika siku
ya pili ya kuhitimisha kwa mkutano ulioshirikisha nchi 13 za Afrika
Mashariki kujadili lengo la nne la elimu kati ya malengo 17 ya maendeleo
endelevu (SDGs).
Alisema
kwamba migogoro ya walimu inayogusa mishahara, marupurupu pamoja na
mazingira bora ya kazi linagusa pia Wizara za TAMISEMI na UTUMISHI na
kusema kwamba wao kama wasimamizi wa elimu watakachoweza kufanya ni
kuzungumza na wenzao kuhakikisha kwamba migogoro hiyo inafutwa ili
utoaji wa elimu uendane na mipango ya kitaifa na kidunia ya lengo la
maendeleo 2030.
Pamoja
na kujibu swali hilo Prof Ndalichako alizungumzia kwamba walimu
walikuwa ni ajenda muhimu na humo walikubaliana kwamba mwalimu ni kila
kitu katika utoaji wa elimu na kuwa hawawezi kufanikiwa katika elimu
bora na jumishi bila kuwa na walimu wenye umahiri, wanaowezeshwa kufanya
hivyo.Kutokana na ukweli huo wamejipanga kuhakikisha kwamba walimu wanapata mafunzo bora na kuwakutanisha kubadilishana uzoefu.
Alisema
kila nchi itakuwa na mpango mkakati wake na kuonesha viashiria kwamba
vinatekelezwa kwa namna gani. Mwisho wa siku mwaka 2030 mataifa yote
yanapaswa kuhakikisha kwamba agenda namba 4 ya maendeleo endelevu ya
elimu imetekelezwa.
Alisema
katika mkutano huo wa siku mbili wa mawaziri wa elimu ulioandaliwa na
UNESCO kwa kushirikiana na ILO, UNFPA, UNDP, UNICEF, UN Women, UNHCR
pamoja na World Bank wamebainisha kwamba mikakati ya pamoja ni lazima
ichukuliwe ili kufanikisha elimu jumuishi yenye usawa na ubora kwa watu
wote huku ikitoa fursa ya elimu kwa wakati wote.
Alisema
kwamba mkutano ulitambua kwamba elimu haina mwisho, elimu inataka kuwa
na mfumo wa kuwa na maendeleo ya kujifunza kwani mambo hayasimami
kutokana na kubadilika kwa teknolojia, hivyo elimu inayotolewa haina
budi kujazia nafasi hiyo kwa kuwapa uhuru watu kujisogeza zaidi.
Alisema
nchi hizo 13 zimekubaliana kwa pamoja kufikia malengo endelevu 2030
kama yalivyosainiwa na kila nchi mwaka 2015 kwa kuweka mikakati ili
mataifa hayo yaweze kufikia malengo yanayotakiwa.
Aidha
alisema kama walikubaliana kwanza kuimarisha elimu ya awali kwa lengo
la kuweka msingi wa kujifunzia, kwani ipo methali inayoaminika kwamba
samaki mkunje angali mbichi na taifa likitaka watoto wasome ni lazima
kuwaanzia wadogo.
Aidha
mataifa hayo yamekubaliana upimaji wa wanafunzi kufanyika kwa ajili ya
kujifunza, ukilenga kutumia matokeo kuandaa mafunzo kwa wanafunzi.
Upimaji uoneshe eneo la ambalo walimu watalazimika kufanya kazi ya ziada
ili wanafunzi wao waelewe.
Mfumo wa sasa wa kupima umelenga kujua watoto wangapi wamefaulu na wangapi wamefeli.
Ndalichako alisema ni vyema upimaji huo kutumika kuimarisha mafunzo ya walimu.
Jambo
la tatu ambalo walikubaliana ni kuhakikisha kwamba mtoto wa kike
anasoma na wale wenye mazingira hatarishi pia; na bila kujali kujali
mazingira yao nchi zinatakiwa kuweka mikakati ya elimu iliyobora kwa
wote.
"Suala
muhimu katika elimu ni kupanga mipango sahihi. Takwimu sahihi ni
changamoto kutokana na ukweli kuwa takwimu hazipatikani kwa wakati au
hazina usahihi au hazifanyiwi uchambuzi katika kufanya maamuzi vizuri, "
alisema Prof Ndalichako.
Pia
mataifa hayo yakiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Sudan Kusini, Ethiopia,
Somalia, Comoro na Djibouti yamesisitiza haja ya kuimarisha elimu nje ya
mfumo rasmi na kwa kuwa kuna mfumo wa elimu wa kujiendeleza wa wakati
wote mfano wa uhasibu.
Alisema
inafaa kuimarisha mifumo ya elimu nje ya mfumo rasmi bila kusahau elimu
ya watu wazima. Pia wametaka watoto wanaolikoroga kwa sababu moja au
nyingine na kujikuta hawapati masomo ni vyema wakarudishwa shuleni
kuendelea na masomo hivyo ipo haja ya kutengeneza mfumo wa kupata elimu
kwa staili hiyo.
"Katika
hili tumekubaliana watoto walionje ya shule wanarudi shuleni au
wanatengeneza mfumo wa kupata elimu" alisema na kuongeza kuwa pia
ilionekana ipo haja ya kuimarisha elimu na ufundi stadi ili elimu hiyo
imwezeshe kujiajiri, kujijenga na kuwa na ujuzi kuendana na soko la
ajira.
Aidha
alisema kwamba kunatakiwa kuanzishwa kwa kampeni maalumu ya kufichua
wasichana wasiopelekwa shule ili kuwepo mwenedelezo wa kila mtu kuingia
shule.WAKATI huo huo serikali ya Uganda imesema itaongeza nguvu katika shule za awali kuimarisha msingi wa utoaji elimu kwa watu wake.
Kauli
hiyo imetolewa na Waziri wa Elimu na shule za msingi wa Uganda, Mh.
Nansubuga Rosemary Seninde wakati akizungumza katika mkutano wa mawaziri
wa Afrika Mashariki kuhusiana na lengo namba 4 la elimu kati ya malengo
17 ya dunia.
Alisema
serikali yake imejikita katika kuhakikisha kwamba waganda wanapata
elimu nzuri na yenye ushindani ikihakikisha ujuzi na uzoefu katika
ujuzi.Aklisema
nchi yake haiwezi kumpa mtu digrii mpaka awe amefanya “intern” na hilo
linasaidia sana kujenga uzoefu wa kile alichosomea.Alisema
ingawa kuna tatizo la bajeti, mipango ni muhimu kuhakikisha kwamba
taifa linatoka katika changamoto za utoaji wa elimu bora.
Alisema
badala ya kusubiri sera, watendaji wanatakiwa kuangalia maeneo ya
kuanzia na kisha kutengenezea taratibu za kubadilishwa kwa sera ili
iendane na kasi inayotakiwa.
SHARE
No comments:
Post a Comment