MAMLAKA
ya Uendelezaji Kanda Maalum za Kiuchumi (EPZA)na Kiwanda kilichopo
ndani ya Mamlaka hiyo ya Tooku kinachojishughulisha na utengenezaji wa
nguo zimetozwa faini ya kiasi cha sh.mill 30 kwa kosa la kutililisha
maji machafu katika makazi ya watu.
Ambapo
EPZA inapaswa kulipa faini ya Mill20 huku Kampuni ya TOOKU kulipa faini
ya mill 10 na kuhakikisha zinarekebisha mifumo yake ya kupitisha maji
taka ipasavyo na kuunganisha katika Mfumo maalum wa Dawasco .
Akizungumza
Jijini Dar es Salaam ,Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-
Mazingira na Muungano,Luhaga Mpina wakati wa ziara yake ya kukagua
baadhi ya viwanda nchini,kuangalia hali ya mazingira ambapo aliambatana
na Maofisa mbalimbali kutoka
Baraza
la Taifa la Hifadhi ya Mazingira (NEMC),alisema faini hizo zinapaswa
kulipwa ndani ya siku 14.Mpina alisema anahasira zaidi na taasisi za
serikali zisizofata sheria ya mazingira na kutililisha maji machafu
katika makazi ya watu.
"Nina
hasira na taasisi hizi za serikali kwani serikali yenyewe haiwezi
kugeuka kupeleka sumu kwa wananchi wake, ambao muda wote inawazuia na
kuwakinga wananchi hao hao wasipatwe na
madhara,"alisema
Alisema
wanapokuta na taasisi ya serikali zinazokiuka miiko iliyoweka katika
utunzwaji wa mazingira ni lazma wawapige faini kubwa zaidi kuliko
taasisi binafsi ili kuweza kuwa mfano mkubwa
kwa jamii.Mpina alisema Mamlaka hiyo ya Uendelezaji Kanda Maalum za
Kiuchumi EAPZ ilisema kuwa mfumo wao wa kuyabeba maji taka na kuyapeleka
katika mfumo rasmi wa maji taka wa Dawasco umeharibika lakini
hawakuweza kuwaandikia NEMC barua ya taarifa juu ya matatizo hayo.
"Nawataka
EPZA ndani ya siku saba mfumo wa kupitishia maji taka wa EPZA uwe
umetengenezwa na kukamilika hivyo kuzuia maji taka yanayotoka kutotoka
tena kwa sababu yatakuwa yanaingia rasmi katika mfumo wa
Dawasco,"alisema.Aidha alisema kwa upande wa Kampuni ya TOOKU yenye
inatakiwa kufanya marekebisho makubwa katika mitambo yake ya kutibu maji
taka kwani inaonekana kuwa na kasoro.
"Sheria
ya mazingira inakataza utililishaji huu wa maji taka katika mazingira
kwani maji yanayotililishwa yanakuwa na kemikali mbalimbali ambazo
zinadhuru wanyama,mimea na maisha ya binadamu,kwahiyo viwanda vyetu
nchini hatuviruhusu kutililisha maji taka nje kwenda kwenye mazingira na
endapo yatatililishwa yanapaswa kupimwa,kuhakikiwa na kudhibitishwa
kuwa hayana madhara,"alisema .
Aidha
alisema katika ukaguzi walioufanya mamlaka hiyo na kiwanda hicho
hakikuweza kuonyeshwa ubora wa maji yanayotililika kuja katika mazingira
ya watu kwani maji yanayotililika kutoka katika Mamlaka hiyo na Kiwanda
hicho cha yanatoka na rangi.
Kwa
Upande wake Mratibu wa Kanda ya Mashariki NEMC , Jafari Chimgege alisema
katika kiwanda cha Tooku kimekuwa mbaya wa kutibu maji taka na
kusababisha kumwaga maji machafu katika mazingira bila kuyatibu ambapo
ni kinyume cha sheria.
"Viwanda
vinafahamu kuwa vinapomwaga maji machafu katika mazingira bila kuyatibu
au kuyapeleka katika mifumo rasmi ni kosa,kiwanda hiki cha TOOKU na
Mamlaka hii ya EAPZ vimefanya kosa,"amesema.Chimgege amesema maji
yanayotilishwa na viwanda mbalimbali
katika mito ni makosa kwani maji hayo yanakuwa na madhara kwa wananchi.
Nae
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Muongozo,James Ngoitanile alisema
wananchi wake wamekuwa wakipata shida na maji hayo wakati mwingine
yanawaletea madhara.Amesema wapo watu wanaolima michicha ambao wanatumia
maji ya mto huo kumwagilia hivyo yanavyochanganyika na maji hayo
yanasababisha watu kula mbogamboga zenye kemikali.
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga
Mpina akiwa katika ziara ya ukaguzi wa Mazingira katika kituo cha
uwekezaji cha EPZA, kilichopo Ubungo Jijini Dar es salaam.
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga
Mpina akiangalia shughuli za uzalishaji wa nguo katika kituo cha
uwekezaji cha EPZA mara baada ya kufanya ziara ya ukaguzi wa mazingira
katika kituo hicho kilichopo Ubungo Jijini Dar es salaam.
.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh.
Luhaga Mpina akiangalia suruali aina ya Jinsi zinazozalishwa katika
kituo cha uwekezaji cha EPZA wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa
mazingira mapema hii leo Jijini Dar es salaam.
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga
Mpina akiangalia mfereji wa maji machafu yanayotiririshwa na kituo hicho
ambayo yamekuwa ni kero kwa wananchi.
SHARE
No comments:
Post a Comment