KUTOKANA na kutangaza mpango wake wa kuzindua maduka zaidi ya 2000 nchi
nzima, kampuni ya
simu za mkononi ya Airtel leo imezindua maduka 15 katika mkoa wa
morogoro kwa lengo la kuhakikisha bidhaa na huduma zake zinawafikia
wateja wake kwa ukaribu na urahisi zaidi
Akiongea
wakati wa uzinduzi , Meneja Mauzo Kanda ya Morogoro, Albert Mtalemwa
alisema “ tunazindua maduka 15 mojawapo likiwa hapa ndani ya kituo
cha mabasi kilichopo Msavu Morogoro
kwa lengo la kuwawezesha wasafiri na wale wanaoingia kutoka maeneo
mbalimbali, wafanyabiashara na wakazi wa Morogoro wanaotembelea kituo
hiki kupata huduma zetu za Airtel husasani huduma ya kifedha kupitia
simu za mkononi kwa urahisi zaidi na wakati wowote.
Maduka
mengi ya Airtel ambayo yanafanya kazi ya kutoa huduma yapo katika
maeneo mbalimbali ambayo ni pamoja na Itigi, Gairo,Kilombero na,mjini,
Kilosa karibu na kituo cha mabasi,
Kimamba mjini, Ruaha, Dumila, Dakawa karibu na soko, Mikese karibu na
mizani, kituo cha Kisaki, Soko la Bwawani, Ifakara mjini na Ifakara
kituo cha basi.
Lengo
letu ni kuziweka huduma zetu karibu na wateja wetu ili kutatua
changamoto zao za mawasiliano kwa wakati na kuwawezesha kupata huduma za
kifedha kwa urahisi. Tunaamini maduka
haya yataongeza idadi ya vituo vyetu na kuboresha kiwango katika huduma
zetu”. aliongeza Mtalemwa
Kwa
upande wake, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, , Maisha Maganga
alisema” nawapongeza sana Airtel kwa mpango huu unaochochea kuboresha
huduma zake kwa wateja lakini pia
kuhakikisha usalama katika huduma za kifedha kupitia maduka haya. Hii
ni fursa pekee kwa kwa wenye maduka kushirikiana na Airtel na kuongeza
mitaji yao lakini pia tunaamini kupitia maduka haya yataongeza ajira
kwa vijana na kuboresha usalama wakazi na pesa
zao kwani sasa wakazi wa maeneo ya hapa yatatunza pesa zao kwenye simu
na kuzitoa kwa urahisi kupitia maduka haya
Uzinduzi
wa maduka ya Morogoro umefatiwa na uzinduzi wa maduka 8 mkoani
Shinyanga wiki iliyopita na huku mpango wake mzima ni kuwa na maduka
mengine kama hayo ya 2000 nchi nzima.
Meneja
Mauzo wa Mkoa wa Pwani, Philiph Nkupama (watatu kushoto) akimweleza
jambo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Maisha Maganga wakati
wa uzinduzi wa duka la Airtel lililopo maeneo ya stendi ya
Msamvu mkoani Morogoro. Ambapo Airtel ilitangaa rasmi maduka 15 mapya
ambayo yanatoa huduma katika maeneo mbalimbali mkoani hapo.
Kaimu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Maisha Maganga akiongea wakati wa
uzinduzi wa duka la Airtel l lililopo maeneo ya stendi ya Msamvu mkoani
Morogoro ambapo Airtel pia ilitangaa rasmi maduka 15 mapya
ambayo yanatoa huduma katika maeneo mbalimbali mkoani humo.
SHARE









No comments:
Post a Comment