Geofrey Tengeneza, Berlin
BANDA la Tanzania katika maonyesho ya Kimataifa ya ITB
yanayoendelea hapa Berlin Ujerumani limeendelea kuwa kivutio kikubwa kwa wageni
wanaotembelea maonesho hayo huku uwepo wa michoro na nyayo za binadamu wa kale
(zamadamu) pamoja na historia yake ikikonga mioyo ya wageni hao.
Sambamba na uwepo wa vielelezo mbalimbali vya vivutio
kadhaa muhimu vya Tanzania kama vile mlima Kilimanjaro, Bonde la Ngorongoro,
wanyama wanaohama katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti n.k, pamoja na maelezo
sawia yatolewayo na Maafisa waandamizi wa TTB kuhusu vivutio hivyo, nyayo za
binadamu wa kale anayesadikiwa kuishi miaka takribani milioni 4 iliyopita
katika eneo la Laetori kilometa 45 kusini mwa Oldvai gorge, imekuwa chachu ya kuvutia wageni
wanaotembelea banda la Tanzania ambao pia wameonesha dhamira kubwa ya
kuitembelea Tanzania.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii
Tanzania Bibi Devota Mdachi pamoja na utangazaji mkubwa wa vivutio mbali mbali
vya utalii vya Tanzania unaofanywa katika maonesho haya, TTB imeamua pia mwaka
huu kuweka mkazo maalumu katika kuitangaza Tanzania kama chimbuko la binadamu
kwa kuleta vielelezo vinavyothibitisha ukweli huo ikiwa ni pamoja na nyayo ya
binadamu wa kale iliyogunduliwa huko Laetoli.
“Nyayo za Laetoli kama ilivyo kwa fuvu la binadamu wa
kale lililovumbuliwa huko Olduvai gorge, ni uthibitisho wa binadamu wa kale
kuishi Tanzania, hivyo tunafurahi kuwa michoro na nyayo tulizokuja nazo
zimewavuti sana wageni na dhamira yetu ni kwamba dunia ijue ukweli huo” alisema
Bi Mdachi.
Jumla ya makampuni 61 kutoka taasisi za umma na
binafsi kutoka Tanzania zinashiriki maonesho ya ITB mwaka huu chini ya
usimamizi TTB. Makampuni kutoka sekta binafsi yanahusisha wasafirishaji watalii
(tour operators,) watoa huduma za usafiri wa anga, watoa huduma za malazi na
kadhalika.
Ujumbe wa Tanzania unaoshiriki maonesho hayo unaongozwa
na Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar Mh. Rashid Ali Juma. Wengine katika ujumbe huo ni pamoja na Balozi wa
Tanzania nchini Ujerumani Mh. Philip Marmo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce Nzuki na Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania
Jaji Mstaafu Thomas Mihayo.
Maonesho ya ITB ambayo ni makubwa kuliko yote duniani
yameanza tarehe 8/3/2017 na yanatarajia kufikiamwisho tarehe 12/3/2017. Kwa
mujibu wa waandaji maonesho yam mwaka huu yamehudhuriwa na nchi 187.
Photo
captions:
Photo 1:
Mchoro wa
binadamu wa kale wakitembea katika eneo la Laetoli lililoko km 45 kusini mwa
Olduvai gorge.
Photo 2
Nyayo wa
binadamu wa kale kama unavyoonekana katika banda la Tanzania katika maonesho ya
ITB.
Photo 3:
Sehemu ya
watu wakiingia kuelekea Banda la Tanzania katika maonesho ya ITB Berlin
Ujerumani.
SHARE
No comments:
Post a Comment