KUNDI linaloongoza katika shughuli za kuhifadhi Tembo limesema kwamba
bei ya pembe za Tembo nchini China imepungua wakati nchi hiyo ikielekea
hatua ya kupiga marufuku kabisa biashara haramu ya pembe hizo mwaka
huu.
Wataalamu wanasema kwamba mahitaji ya pembe za Tembo nchini China ni chanzo kikubwa cha kusababisha hatari ya kutoweka kabisa kwa wanayama hao.
Shirika la Save the Elephants limezindua ripoti yake leo ambayo imelenga utafiti uliofanyika juu ya bei ya pembe za Tembo katika masoko kote China katika kipindi cha miaka mitatu na kubaini kwamba imepungua kutoka dolla 2,100 kwa kilo mwanzoni mwa mwaka 2014 hadi dolla 730 mwezi Februari mwaka huu.
Shirika hilo linasema kilichosababisha hali hiyo ya kupungua kwa bei ya pembe za ndovu ni pamoja na ukuaji mdogo wa kiuchumi hali ambayo imechangia watu wachache kumudu kununua bidhaa za kifakhari, pamoja na kuandamwa kwa watu wanaofanya biashara zinazofungamana na rushwa na kuzuiwa kununua bidhaa zinazotokana na pembe za ndovu za gharama kubwa ambazo huzitowa kama takrima kwa maafisa wa serikali.

No comments:
Post a Comment