Denmark imeungana na nchi kadhaa kuzuia juhudi za Uturuki kufanya
kampeni kwenye nchi za Ulaya. Waziri Mkuu wa Denmark, Lars Lokke
Rasmussen amependekeza kwa mwenzake wa Uturuki, Binali Yildrim
kuahirisha ziara yake nchini Denmark kutokana na mvutano unaoendelea
kati ya Uturuki na Uholanzi. Kituo cha utangazaji cha Denmark, DR,
kimeripoti kuwa Yildirim alipanga kuzuru Denmark tarehe 20 ya mwezi huu
wa Machi, lakini Rasmussen amesema kwamba ziara kama hiyo inaweza
isifanyike kutokana na hatua ya hivi karibuni ya Uturuki kuishambalia
Uholanzi kwa maneno. Uturuki inazozana na nchi kadhaa za Ulaya kutokana
na jaribio lake la kutaka kuendesha mikutano ya hadhara ili kufanya
kampeni kwa Waturuki walioko nje ya nchi kwa ajili ya kupiga kura ya
'Ndiyo' katika kura ya maoni inayotarajiwa kufanyika mwezi Aprili kwa
ajili ya kumuongezea mamlaka zaidi Rais Recep Tayyip Erdogan.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment