Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia watoto UNICEF, limesema
mamia ya watoto wameuawa nchini Syria kwa mwaka 2016. UNICEF imetangaza
leo kuwa idadi hiyo ndio kubwa zaidi kuwahi kurekodiwa tangu shirika
hilo lianze kuhakiki idadi ya vifo katika mgogoro huo. Kwa mujibu wa
UNICEF, kiasi ya watoto 652 wamekufa katika mzozo unaoendelea nchini
Syria, ambao Jumatano ijayo mzozo huo utaingia mwaka wake wa sita. Mkuu
wa UNICEF katika ukanda wa Mashariki ya Kati, Geert Cappelaere amesema
mateso yasiyokuwa ya kawaida yameshuhudiwa. Ripoti hiyo ya UNICEF
imesema shule, hospitali, viwanja vya michezo na maeneo mengine ya
watoto kwa kawaida yamekuwa yakilengwa na mashambulizi. Shirika hilo
limesema kiasi ya watoto 255 wameuawa katika maeneo yaliyo karibu na
shule kwa mwaka 2016. Watoto milioni sita nchini Syria wanategemea
msaada wa kibinaadamu, lakini kiasi ya watoto 250,000 bado wako kwenye
maeneo yaliyozingirwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment