Mgombea urais wa chama cha kihafidhina cha Ufaransa Francois Fillon
amefanya mkutano uliohudhuriwa na maelfu ya wafuasi wa chama hicho cha
Republicain mjini Paris jana, na kuapa kuendelea na kampeni yake licha
ya kwamba maafisa wengi wa chama chake wamemtupa mkono. Alipoulizwa
ikiwa ataisimamisha kampeni yake, bila kusita amesema jibu ni hapana, na
kuongeza kuwa hakuna mtu atakayemzuia kuendelea katika kinyang'anyiro
cha urais. Fillon ambaye wakati mmoja aliongoza katika kura za maoni,
anakabiliwa na tuhuma za kutumia vibaya fedha za umma. Inaaminika kuwa
mgombea huyo atafunguliwa mashitaka rasmi, baada ya polisi kuipekuwa
nyumba yake wiki iliyopita na korti kumteuwa jaji atakayechunguza tuhuma
dhidi yake. Fillon anasema tuhuma hizo zina malengo ya kisiasa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment