TRA

TRA

Wednesday, March 22, 2017

Jaji Gorsuch asema Trump hayuko juu ya sheria Marekani

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !

JAJI aliyependekezwa na Rais wa Marekani Donald Trump kujaza nafasi iliyo wazi katika Mahakama ya Juu nchini humo, amesema hakuna mtu yeyote aliye juu ya sheria, hata Rais Trump aliyependekeza uteuzi wake.

Neil Gorsuch ameambia kikao cha bunge la Seneti kwamba hakuna mtu yeyote aliyemtaka kutoa ahadi kuhusu jinsi atakavyofanya maamuzi yake pindi atakapoidhinishwa kuwa jaji katika mahakama hiyo.
Amesema angekataa uteuzi huo iwapo Trump angemtaka kubatilisha uamuzi wa kihistoria wa mahakama katika kesi Roe v Wade ambao ulihalalisha utoaji wa mimba.
Gorsuch pia alishutumu vikali hatua ya Trump kuwashambulia kwa maneno majaji wa mahakama mara kwa mara na kusema "inavunja moyo".
Februari, rais huyo alimweleza jaji aliyebatilisha marufuku yake ya usafiri dhidi ya raia wa nchi saba kama "mtu huyo anayeitwa jaji".
Gorsuch faraghani aliwaambia maseneta kwamba hilo lilikuwa na maana kwamba iwapo kungetokea shambulio la kigaidi katika ardhi ya Marekani, basi jaji huyo ndiye angekuwa lawamani.
"Mtu yeyote anapokosoa uaminifu na maadili au nia ya jaji wa mahakama, hilo linavunja moyo. Nafikiri linatamausha - kwa sababu naujua ukweli," alisema.
Alipoulizwa iwapo hilo linamhusu pia rais, alijibu: "Mtu yeyote ni mtu yeyote."
Msemaji wa ikulu ya White House Sean Spicer baadaye aliandika kwenye Twitjer kwamba Bw Gorsuch alikuwa akizungumza "kwa mapana" na kwamba hakumtaja mtu kwa jina."
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maandamano dhidi ya Neil Gorsuch 15 Machi
Wakati wa kikao chake cha kwanza kuhojiwa na maseneta, Gorsuch, ambaye ni jaji wa Colorado aliulizwa maswali mengi kuhusu msimamo wake.
Maseneta wa Democrat walisisitiza kuhusu baadhi ya mambo yenye utata, lakini alisisitiza mara kwa mara kwamba ingekuwa makosa kwake kueleza angetoa uamuzi wa aina gani katika kesi yoyote hilo.
Alisema huo ungekuwa ndio "mwanzo wa mwisho" wa mahakama huru.
Bw Gorsuch, amependekezwa kujaza nafasi iliyoachwa wazi kutokana na kifo cha Jaji Antonin Scalia miezi 13 iliyopita.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger