Baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul
Makonda kuvamia ofisi za Clouds TV na kuwalazimisha watangaza wa kipindi
cha Shilawadu kurusha kipindi kinachomuhusu Askofu Gwajima kikiwa
hakijamaliziwa maandalizi kinyume na taaluma ya habari, Leo March 22,
2017 Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limefanya kikao cha maamuzi dhidi
suala hilo.
TEF
pamoja na Club ya Waaandishi wa Habari Dar es saalam (DCPC) na Umoja wa
Club za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) zimepitisha maamuzi matatu
ikiwemo.
- Kulaani vikali vitendo vya RC Paul Makonda
- Kutoandika na kutangaza habari zozote kuhusu Paul Makonda kwenye chombo chochote cha Habari.
- Kumtangaza RC Makonda kama adui wa Uhuru wa Vyombo vya Habari pamoja na yeyote atakayeshirikiana naye.
Unaweza kusoma kila kitu kwenye tamko hili hapa chini.
SHARE
No comments:
Post a Comment