Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akimkaribisha
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii,
Mhe. Peter Serukamba (kulia) pamoja na Wajumbe wengine mara baada ya
kuwasili katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) kwa
ajili ya kukagua mradi wa ukarabati wa taasisi hiyo, 17 Machi, 2017.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akiwa
ameongozana na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na
Maendeleo ya Jamii, Mhe. Peter Serukamba pamoja na Wajumbe wengine mara
baada ya kuwasili katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA)
kwa ajili ya kukagua mradi wa ukarabati wa taasisi hiyo, 17 Machi,
2017.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA), Dkt.
Helbert Makoye akiwaeleza jambo Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Huduma na Maendeleo ya Jamii, mara baada ya kuwasili katika taasisi hiyo
kwa ajili ya kukagua mradi wa ukarabati wa taasisi hiyo, 17 Machi,
2017.
Mkuu
wa Kitengo cha Muziki wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA)
Bi.Rhoda Mitanda (kushoto) akiwaeleza Wajumbe wa Kamati ya Kudumua ya
Bunge ya Huduma na Maendeleo kuhusu namna vifaa mbalimbali vya muziki na
kazi zake mara walipowasili katika Taasisi hiyo kwa ajili ya kukagua
mradi wa ukarabati wa taasisi hiyo, 17 Machi, 2017.
Wajumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii,
wakionyeshwa vifaa vitumikavyokatika uhariri wa kazi za sanaa
walipoingia katika moja ya Studio ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni
Bagamoyo (TaSUBA) kujionea utendaji kazi wa taasisi hiyo, 17 Machi,
2017.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Mhe.
Peter Serukamba akiongea na Wafanyakazi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni
Bagamoyo (TaSUBA) mara baada ya kuwasili katika Taasisi hiyo kwa ajili
ya kukagua mradi wa ukarabati wa taasisi hiyo, 17 Machi, 2017.
Wajumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii pamoja na
Wafanyakazi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA)
wakijadiliana wakati wa kikao 17 Machi, 2017.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akiongea na
Wafanyakazi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) wakati wa
kikao cha kukagua mradi wa ukarabati wa taasisi hiyo, 17 Machi, 2017.
Baadhi
ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii
wakitoa maoni yao wakati wa kikao cha kujadili na kukagua mradi wa
ukarabati wa taasisi hiyo, 17 Machi, 2017.
Baadhi
ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii
pamoja na Wafanyakazi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo
(TaSUBA) wakisikiliza maoni mbalimbali yaliyolenga kuiboresha taasisi
hiyo wakati wa kikao cha kujadili na kukagua mradi wa ukarabati wa
taasisi hiyo, 17 Machi, 2017.
Wanafunzi
wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) wakionyesha umahiri
wao katika sanaa mbalimbali mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii baada ya kumalizika kikao
kilicholenga kukagua mradi wa ukarabati wa taasisi hiyo, 17 Machi,
2017.
Wajumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakiwa
katika picha ya pamoja na Wafanyakazi pamoja na Wanafunzi wa Taasisi ya
Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) mara baada ya kumalizika kwa ziara
iliyolenga kufanya ukaguzi wa mradi wa ukarabati wa taasisi hiyo, 17
Machi, 2017. (Picha/Habari na Benedict Liwenga-WHUSM)
KAMATI
ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii imeipongeza Taasisi
ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) kwa juhudi zake inazozifanya
katika kuibua na kukuza vipaji vya Vijana nchini.
Pongeza
hizo zimetolewa leo Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani na Wajumbe wa Kamati
hiyo wakati walipoitembelea taasisi hiyo kwa ajili ya kukagua mradi wa
ukarabati wa taasisi hiyo.
Akiongea
wakati wa kikao na Watendaji wa Taasisi hiyo, Mwenyekiti wa Kamati
hiyo, Mhe. Peter Serukamba amesema kwamba, suala la muziki, filamu na
utamaduni ni suala la kipaji, hivyo halihitaji elimu kubwa kwa vijana,
bali kuwepo na mazingira mazuri yatakayowezesha wenye vipaji na wasio na
vipaji waweze kupata fursa ya kujifunza na kuonyesha vipaji vyao.
Mhe.
Serukamba amelishauri Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) kuweka mazuri
ambayo hayatawabana vijana ambao hawakupata fursa ya elimu lakini wana
vipaji, hivyo ameshauri vijana nchini wapewe fursa ya kujifunza na
vipaji vyao viendelee kuibuliwa.
Sambamba
na hilo, Mhe. Serukamba ameishauri taasisi hiyo kutoa elimu ya lugha
mbalimbali kama vile lugha za Kiingereza, Kiswahili, Kifaransa,
Kijerumani, Kichina na nyinginezo ili ziweze kuwasaidia vijana hao
wawapo nje ya nchi na pindi wanapokuwa wameiva katika masomo yao ndani
ya chuo hicho.
“Chuo
hiki naomba kione namna ya kufundisha lugha pamoja kwamba mnafundisha
muziki, basi vema mkawafundisha vijana wetu lugha mbalimbali ili waweze
kwenda Duniani, kwasababu kama watakuwa na tatizo la lugha itawapa
shida”, alisema Serukamba.
Kuhusu
suala la bajeti katika taasisi hiyo, ameshauri kwamba, Uongozi wa
taasisi hiyo haunabudi kujitangaza ili waweze kupata fedha za kutosha
badala ya kulalamika kwamba hawana fedha.
“Lazima
Mkuu wa Chuo uende mbali zaidi kwasababu vitu mnavyofundisha hapa
katika taasisi yenu ni vya kipekee, havifundishwi kwingine, hivyo una
fursa kubwa ya kujitangaza na kuweza kupata fedha za kukisaidia chuo
hiki, kwa mfano unaweza kuwatafuta watu toka sekta binafsi ambao hawa
wataweza kukusaidia kama vile makampuni mbalimbali hapa nchini”,
aliongeza Serukamba.
Kwa
upande wake Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Nape
Nnauye amesema kwamba, moja ya changamoto kubwa ambayo imekuwa
ikiikabili taasisi hiyo ni mmomonyoko wa kingo za mpaka wa taasisi hiyo
ambao umesababishwa na bahari kusogelea eneo la taasisi hiyo hali ambayo
inahatarisha majengo yake, hivyo amefafanua kuwa tayari Wizara
iliwasiliana na Ofisi ya Makamu wa Rais upande wa Mazingira ambao wao
tayari walifika na kupima athari za mmonyoko huo.
Ameongeza
kuwa, kwa hivi sasa kinachosubiriwa ni fedha ambazo zitatumika kuanza
ujenzi wa kingo ambayo itasaidia kuepusha mmomonyoko huo unaofanywa na
maji ya bahari.
“Hili
eneo la taasisi ya TaSUBA watu wa NEMC walishafika na kupima na
tunategemea katika mwaka ujao wa fedha, fedha itapatikana ili kuanza
ujenzi wa kingo katika eneo hili ili tuweze kuzuia maji ya bahari
kuendelea kuharibu eneo la taasisi hii”, alisema Mhe. Nnauye.
Kuhusu
suala la elimu itolewayo katika taasisi hiyo, amesema kwamba
anakubaliana na mapendekezo ya Kamati kwamba, vijana wapewe fursa ya
kufundishwa kwa kuangalia vipaji vyao na isiwe lazima sana kuangalia
elimu waliyonayo kwani wako vijana wengi ambao wana vipaji lakini
hawakupata fursa ya kuelimika, lakini pia na wale walioelimika wanayo
nafasi ya kujifunza ndani ya chuo hiko.
Awali
akitoa taarifa ya taasisi hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo,
Dkt. Helbert Makoye amesema kwamba, taasisi anayoiongoza ni taasisi
iliyotukuka na inafundisha masuala mbalimbali ya Sanaa, inakuza viwango
vya Sanaa, inakuza matumizi ya Sanaa kama vile maonyesho mbalimbali
yenye kutoa elimu kwa jamii.
“Hapa
chuoni pia tunafundisha watendaji kwenye masuala ya Sanaa lakini pia
Wasimamizi, tunawandaa Watafiti na Washauri wa Sanaa na utamaduni kwa
ngazi ya Taifa na Kimataifa”, alisema Dkt. Makoye.
SHARE
No comments:
Post a Comment