Kituo
namba moja kwa vijana East Africa Television (EATV) Limited
kikishirikiana na Taasisi ya Haki za Wanawake (HAWA foundation)
kinapenda kutoa shukrani za dhati, kwa umma wa
watanzania kwa kufanikisha kuchangia kwenye kampeni ya Namthamini.
Namthamini ni
kampeni iliyolenga katika kuchangia pedi (Taulo za Kike) kwa
wanafunzi wa Sekondari, kutokana na takwimu kuonesha karibia asilimia
45 ya wanafunzi wa kike hukosa masomo wakiwa katika hedhi kutokana na
kukosa pedi za kujistiri.
Kwa
wastani wanafunzi wa kike wengi hupoteza siku tano hadi saba kila mwezi
kutokana na ukosefu wa pedi za kujisitiri, na kwa mwaka inakadiriwa
kukosa masomo kwa takribani siku 60 hadi 70.
EATV
na East Africa Radio katika kufikisha mchango wake kwa jamii, na kwa
kuangalia Siku ya Wanawake Duniani, Machi mosi tuliamua kuanzisha
kampeni hii kwa kuishirikisha jamii ili kumuwezesha mwanafunzi wa kike
asikose masomo yake na kumfanya kutofikia lengo lake kimasomo kwa kukosa
pedi pale awapo kwenye hedhi.
EATV
na East Africa Radio pamoja na Taasisi ya Haki za Wanawake (Hawa
Foundation) imefanikiwa kukusanya michango ya fedha taslim na pakiti za
pedi zitakazowawezesha takribani wanafunzi wa kike wapatao 673
kutokukosa masomo yao kwa muda wa mwaka mzima.
Katika
kampeni hii ambayo wananchi walijitokeza kuichangia katika kuonyesha
kumjali mtoto wa kike aliyepo shuleni zilichangwa jumla ya shilingi
20,176,110, ambazo fedha taslim shilingi 11,774,610 na pedi za thamani
ya shilingi 8,401,500.
Michango
yote ya fedha iliyopatikana itatumika katika kununua pedi na
zitaelekezwa moja kwa moja katika shule za Sekondari 20 zenye uhitaji
zilizoteuliwa kupata msaada huu, katika mikoa ya Morogoro, Iringa,
Lindi, Pwani na Tanga.
Uongozi
wa EATV Limited na Taasisi ya Haki za Wanawake (Hawa Foundation)
inapenda kutumia nafasi hii kwa dhati kuwashukuru wananchi wote
walioguswa na tatizo la pedi kwa wanafunzi wa kike na kuichangia kampeni
ya Namthamini na kuonyesha kuwa kwa pamoja tunaweza. Sisi EATV husema
Together Tunawakilisha.
Mwisho
kabisa tunapenda kusisitiza kuwa tatizo la wanafunzi wa kike kukosa
kuhudhuria shuleni kutokana na kukosa pedi za kujisitiri ni la kwetu
sote hivyo East Africa Television Limited pamoja na Taasisi ya Haki za
wanawake inatoa wito kwa jamii kuendelea kuungana kwa pamoja katika
kusaidia watoto wa kike kupata mahitaji muhimu wawapo shuleni, ili
wapate kusoma kwa amani pasipo kukosa kuhudhuria darasani.
Afisa
Masoko wa East Afrika Radio Basilisa Biseko akizungumza mbele ya
waandishi wa Habari (hawapo pichani),mapema leo jijini Dar,kuhusua
mafanikio yaliyopatikana kupitia kampeni ya 'NAMTHAMINI',Basilisa
amebainisha kuwa kupitia EATV
na East Africa Radio pamoja na Taasisi ya Haki za Wanawake (Hawa
Foundation) imefanikiwa kukusanya michango ya fedha taslim na pakiti za
pedi zitakazowawezesha takribani wanafunzi wa kike wapatao 673
kutokukosa masomo yao kwa muda wa mwaka mzima.Pichani kulia ni Mratibu
wa Vipindi Eastafrika Radio,Irene Tillya na kushoto ni Mratibu wa
Vipindi EATV,Sophie Proches.
Mkurugenzi
wa Taasisi ya Haki za Wanawake (HAWA) , Joyce Kiria akifafanua jambo
kuhusiana na mafanikio makubwa waliyoyapata kupitia kampeni hiyo ya
'NAMTHAMINI',Kiria emesema kuwa Katika kampeni hiyo ambayo wananchi
walijitokeza kuichangia katika kuonesha kumjali mtoto wa kike aliyepo
shuleni zilichangwa jumla ya shilingi 20,176,110, ambazo fedha taslim
shilingi 11,774,610 na pedi za thamani ya shilingi 8,401,500.
Afisa
Masoko wa East Afrika Radio Basilisa Biseko akifafanua zaidi mbele ya
Waandishi wa habari (hawapo pichani),kuhusiana na mafanikio ya kampeni
hiyo 'Namthamini',iliyolenga katika kuchangia pedi (Taulo za Kike) kwa
wanafunzi wa Sekondari,ambapo takwimu zinaeleza kuwa karibia asilimia 45
ya wanafunzi wa kike hukosa masomo wakiwa katika hedhi kutokana na
kukosa pedi za kujistiri.
Baadhi ya Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo uliofanyika mapema leo jijini Dar.
SHARE
No comments:
Post a Comment