Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze, Edes Lukoa akizungumza. (picha na Mwamvua Mwinyi)
Mbunge wa jimbo la
Chalinze, Ridhiwani Kikwete akizungumza na madiwani wa halmashauri hiyo
katika baraza la madiwani. (picha na Mwamvua Mwinyi)
Na Mwamvua Mwinyi,Chalinze
HALMASHAURI ya Chalinze
wilayani Bagamoyo mkoani Pwani, imefanikiwa kudhibiti wadudu aina ya
viwavijeshi wanaoharibu mazao mbalimbali ambapo waliingia katika baadhi
ya maeneo mwanzoni mwa mwezi huu.
Aidha wakulima katika halmashauri hiyo wameombwa kuwa wakitoa taarifa mapema mara wanapobaini wadudu hao kushambulia mazao yao.
Akizungumzia kuhusiana
na hali ilivyokuwa na namna walivyochukua hatua, Mkurugenzi wa
halmashauri ya Chalinze, Edes Lukoa aliipongeza serikali kwa hatua
zilizochukuliwa.
Alisema wadudu hao waliingia katika mashamba ya wakulima kuanzia mwanzo wa mwezi wa tatu 2017.
Lukoa alitaja maeneo
yaliyokubwa na changomoto hiyo kuwa ni Msoga, Talawanda, Mkange,
Vigwaza, Msata, Kibindu, Kiwangwa ambako baada ya kutoa taarifa
wataalamu walikwenda na kuangamiza vidudu hivyo.
“Tunashukuru wakati taarifa hizo zinatolewa tayari tulikuwa na chupa 51 zilizoangamiza viwavijeshi katika hekari 3,500″alisema.
Hata hivyo baadhi ya
madiwani walishukuru kwa hatua zilizochukuliwa kusaidia wakulima lakini
wameomba ziongezwe dawa nyingine ili kumaliza kero hiyo katika maeneo
ambayo bado hayajafikiwa kikamilifu.
Kufuatia hoja hiyo, Lukoa alielezea kwamba tayari halmashauri hiyo imepokea chupa 100 za sumu ya kuangamiza maeneo yaliyobakia.
Alisema anauhakika chupa zilizoongezeka zitamaliza kabisa adha hiyo kwa wakulima.
Nae afisa kilimo wa
Halmashauri ya Chalinze, Seth Mgonja alisema ipo mikakati waliojiwekea
kudhibiti kero hiyo mara itakaojitokeza wakati mwingine.
Mgonja alisema wametoa
maelekezo kwa wakulima kutoa taarifa haraka wakishaona wadudu hao na
kuchimba mashimo makubwa endapo wakibaini kuingia kwenye maeneo yao.
Viwavijeshi ni watoto wa vipepeo na kabla ya kukua huwa wakila mazao wakati wa hatua ya lava .
Wadudu hao hula na kumaliza hata shina zima la zao na wanatabia ya kuhama hama
SHARE
No comments:
Post a Comment