Maharamia wa Kisomali wamewaachia mabaharia wanane wa Sri Lanka
waliokuwamo katika meli ya mafuta waliyoiteka nyara. Kwa mujibu wa
taarifa ya walinzi wa pwani ya Puntland, gavana wa jimbo lililohusika na
mkasa huo alifanikiwa kufanya mazungumzo na watekaji nyara ili
mabaharia wa meli hiyo waachiwe bila ya kuwalipa maharamia hao kitita
cha fedha. Meli hiyo ya mafuta ilitekwa nyara jumatatu wakati ilipokuwa
njiani kutoka Djibouti kuelekea Mogadishu. Kwa mujibu wa taarifa meli
hiyo ilisafiri bila ya kusindikizwa na walinzi.
Friday, March 17, 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment