TRA

TRA

Tuesday, March 21, 2017

Mji wa Damascus washambuliwa upya na waasi

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
Waasi na wapiganaji wa jihad wameanzisha operesheni mpya mashariki ya mji mkuu wa Syria Damascus siku mbili baada ya vikosi vya serikali kuzima shambulizi la kwanza kilomita chache kutoka katikati ya mji huo.

Mlipuko mkubwa umeripotiwa kutokea leo alfajiri katika eneo hilo na kufuatiwa na makabiliano makali, mashambulizi ya makombora na mashambulizi ya kutokea angani ya majeshi ya serikali katika maeneo ya upinzani. 

Shirika rasmi la habari la Syria SANA limeripoti kuwa watu 12 wamejeruhiwa katika mashambulizi hayo ya waasi. 

Mapigano hayo mapya yamefanyika siku mbili kabla duru mpya ya mazungumzo ya amani yanayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa yaliyopangwa kufanyika mjini Geneva, Uswisi.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger