UTAWALA wa Marekani unatowa vitisho vipya vya kutaka kuzuia au
kuzifutilia mbali hazina za fedha zinazokusudiwa kusaidia shughuli za
utawala wa sheria katika jamii ambazo zinakataa kushirikiana na juhudi
za serikali kuu za kutaka watafutwe na kurudishwa makwao wahamiaji
kinyume cha sheria.
Tangazo la Mwanasheria mkuu Jeff Session wiki hii
liliyachanganya masuala mawili yanayohusiana na mpango huo wa kuvamia
kile kinachoitwa miji inayowaficha wahamiaji.
Alisema wizara ya sheria
ya Marekani itainyima fedha miji ambayo inakiuka sheria ya nchi
kuhusiana na utoaji na ubadilishanaji wa taarifa miongoni mwa polisi na
mamlaka za serikali kuu.
Kadhalika alitoa tamko la kulaani miji ambayo
inakataa kuzingatia maombi ya kuwa na vituo vya kuzuia wahamiaji.
Aidha
Sessions ametoa maelezo mafupi kuhusu jinsi wizara ya sheria
itakavyopitisha uamuzi juu ya miji ipi inayohusika na hatua gani
zitachukuliwa kuifutia miji hiyo fedha.
No comments:
Post a Comment