BALOZI wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Nikki Haley amesema
upigaji marufuku wa silaha za nyuklia ni jambo lisilowezekana.
Haley aliyasema hayo wakati zaidi ya nchi 100 zilipoanza mazungumzo mjini New York yanayolenga kutafuta njia za kuangamiza silaha za nyuklia duniani.
Nchi 40 hazikushiriki mkutano huo wa Umoja wa Mataifa. Dola kuu zinazomiliki nyuklia zikiwemo Marekani, Uingereza, Ufaransa, Israel na Urusi hazikuhudhuria mkutano huo baada ya kupiga kura kupinga mapendekezo ya mkataba wa kuzipiga marufuku silaha za nyuklia utakaokuwa na mafungamano ya kisheria.
Sweden, Mexico na Afrika Kusini ni miongoni mwa mataifa yanayotaka marufuku kamili ya silaha za nyuklia.

No comments:
Post a Comment