SHIRIKA la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limesema
mamia ya raia wameuawa katika mji wa Mosul nchini Iraq.
Kwa mujibu wa shirika hilo mauaji hayo yalitokea katika miezi ya
hivi karibuni baada ya maofisa kuwaamuru wabakie majumbani mwao licha ya
mashambulizi ya kutokea angani ya muungano unaoongozwa na Marekani
dhidi ya kundi linalojiita Dola la Kiislamu mjini humo.
Raia hadi 150
waliuliwa katika shambulizi la kutokea angani Machi 17 katika kitongoji
cha al-Jadida mjini Mosul.
Shirika hilo limesema agizo la maafisa wa Iraq
lina maana vikosi vya muungano vilitakiwa kufahamu idadi kubwa ya raia
wangekuwa wahanga wa mashambulizi yoyote ya kutokea angani.
Shirika la
Amnesty International linasema kushindwa kuyazuia mashambulizi hayo
huenda kumevunja sheria za kimataifa. Maafisa wa Marekani na Iraq
wanachunguza shambulizi hilo pamoja na mengine.
No comments:
Post a Comment