TRA

TRA

Friday, March 10, 2017

MBUNGE WA KIBAHA MJINI KOKA AHAHIDI KULITATUA TATIZO LA MAJI KWA WAKAZI WA KATA YA PANGANI

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


KIBA
Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka akizungumza na wananchi wa kata ya Pangani baada ya kufanya ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kuweza kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili.
KIBA 1
Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka akiwawahutubia wananchi wa kata ya pangani katika mkutano wa adhara baada ya kufanya ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kukagua miradi ya maendeeo.
KIBA 2
Baadhi ya wananchi wa kata ya pangani katika halmashauri ya Wilaya ya Kibaha mji wakimsikiliza Mbunge wakati akiwahutubia katika mkutano wa adhara uliofanyika katika viwanja vya mtaa wa kidimu.
KIBA 3
Diwani wa kata ya Pangani Agustino Mdachi akifafanua jambo kwa wananchi katika mkutano huo uliondaliwa na mbunge ikiwa ni moja ya ziara yake ya kikazi.
(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU).
………….
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA  
WAKINAMAMA wa kata ya Pangani wanaoishi katika mitaa minne ya Lumumba,Kidimu, Liwale pamoja ma mkombozi katika halmashauri ya Wilaya ya Kibaha mji Mkoa wa Pwani wanakabiliwa na kero kubwa ya ukosefu wa maji safi na salama hivyo kuwalazimu wakati mwingine kuamka usiku  wa manane kwa ajili ya kwenda kuchota maji visimani  kitu ambacho kinahatarisha  usalama wa maisha yao kutokana na mazingira yenyewe kuwepo katika mapori.
Kilio hicho cha wakinamama hao wamekitoa baada ya Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka kufanya ziara yake ya kikazi katika mitaa mbali mbali iliyopo katika kata ya Pangani kwa lengo ya kuweza kufanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo na kuweza kuzungumza na wananchi ili kubaini changamoto ambazo zinawakabili.
Wakinamama hao akiwemo Maria Benjamini ,Zawadi Ibrahimu,pamoja na Asimu Mendani  walisema kuwa wanashindwa kufanya shuguli nyingine za kuleta maendeleo kutokana na kutumia muda mwingi wa kutafuta maji hivyo wameiomba serikali kupitia mamlaka zinazohusika  kuliingilia kati suala hilo kwa lengo la kuweza kuwapatia huduma ya maji.
Kilio cha wakinamama hao kinamgusa na kumwinua  Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka na kuamua kumwagiza mbele ya mkutano wa adhara  Injinia wa maji katika halmashauri ya Wilaya ya Kibaha mji kuhakikisha wananchi wa mitaa minne ya Kidimu, Lumumba,miwale pamoja na mkombozi iliyopo kata ya Pnagani wanapata maji ya bomba  haraka ili waweze waondokana na adha waliyokuwa wanakabiliana nayo kwa muda mrefu.
Koka alisema kwamba suala hilo hawezi kulifumbia macho hata kidogo na atahakikisha kwamba analivalia njuga kwa lengo la kuweza kuona wananchi wake wa kata ya Pangani wanapata maji safi na salama na kuondokana na adha ambayo wamekuwa wakiipata kwa kipindi cha muda mrefu.
“Ndugu zangu wananchi wa kidimu ninachotaka kusema ni kwamba ninamwagiza Injinia wa maji kuhakikisha kwamba katika mitaa yote minne maji yanapatikana ili wananchi waweze kuondokana na usumbufu huu hususan wakinamama wanaamka nyakati za usiku kwenda kutafuta maji kitu ambacho mimi kama Mbune wenu sitaki kukiona ninachotaka ni maji,”alisema Koka.
Akijibu malalamiko yaliyotolewa na wananchi hao wa pangani Mbele ya Mbunge  kuhusina na kilio chao cha siku nyingini juu ya kero  sugu ya upatikanaji wa maji Injinia wa halmashauri ya Wilaya ya Kibaha mjini Grace Limo amesema kuwa  kwa sasa taratibu zote zimeshafanyika la kuweka bomba kubwa ambalo litakiuwa likisambaza maji  katika maeneo mbali mbali ya Kibaha kutoka mtambo wa Ruvu juu.
KUWEPO kwa tatizo sugu  la upatikanaji wa maji safi na salama kwa wakazi wa kata ya Pangani katika halmashauri ya Wilaya ya Mji wa Kibaha kusababisha baadhi ya wakinamama kuacha familia zao wakiwemo watoto watogo  nyakati za usiku kwa ajili ya kwenda kuchota maji  hivyo kunahitajika juhudi za makusudi kutoka serikali katika kulitafutia ufumbuzi wa kudumu suala hilo.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger