Klabu ya Arsenal imepanga
kumtengea donge nono la mshahara Mesut Ozil ikiwa ni ofa nono ya
mshahara unaofikia paundi 280,000 kwa wiki ili aweze kubakia katika
klabu hiyo.
Kiungo huyo wa kimataifa wa
Ujerumani bado hajaamua kuhusu mustakabali wake huku ikiwa imebaki miezi
15 katika mkataba wake wa sasa, na kumekuwa na wasiwasi uliobuka kuwa
anaweza kuondoka msimu huu wa kiangazi.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28
tayari ndio mchezaji anayelipwa zaidi Arsenal akikunja kitita cha
paundi 140,000 kwa wiki ambazo zinaongezeka mpaka kufikia paundi 200,000
kwa wiki huku akiongeza na bakshishi.
Arsenal wako tayari kumuongeza
zaidi lakini Ozil anaonekana kutokuwa tayari akifahamu kuwa anaweza
kupata zaidi akienda kwingine.
SHARE
No comments:
Post a Comment