Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu amesema kuwa
atakwenda nchini Uholanzi leo hii kuhutubia mkutano wa hadhara ili raia
wa Uturuki wanaoishi nchini humo waunge mkono kura ya maoni yenye lengo
la kumuongezea mamlaka rais Recep Tayyip Erdogan. Cavusoglu
alipozungumza na waandishi wa shirika la habari la CNN alisema atakwenda
mjini Rotterdam kukutana na wafuasi wa rais Erdogan na ameonya kuwa
iwapo serikali ya Uholanzi itamkataza kuingia nchini humo basi Uturuki
itaiwekea nchi hiyo vikwazo vikali. Cavusoglu pia ameeleza kwamba hatua
ya Ujerumani na Uholanzi ya kupiga marufuku kampeni ya kuunga mkono kura
ya maoni itakayofanyika April 16 juu ya kuibadilisha katiba ya Uturuki
ina maana kwamba nchi hizo zinaunga mkono wapinzani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment