Katika hatua ya karibuni ya mgogoro wa kidiplomasia, Ujerumani jana
imeionya kwa hasira Uturuki ikisema Rais Recep Tayyip Erdogan amekwenda
mbali baada ya kumtuhumu kansela Angela Merkel kwa kutumia "hatua za
kinazi." Uturuki na Umoja wa Ulaya zimo katika mgogoro unaotishia
kudhoofisha juhudi za Uturuki kujiunga na Umoja wa Ulaya, wakati ambapo
mzozo unazidi kuelekea kura ya maoni ya Aprili 16, kuhusu kuongeza
mamlaka ya Rais Erdogan. Mgogoro huo ulizuka baada ya maafisa wa
Ujerumani na mataifa mengine ya Umoja wa Ulaya kukataa kuwaruhusu baadhi
ya mawaziri wa Uturuki kupga kampeni ya "Ndiyo" katika ardhi za mataifa
hayo, na hivyo kusababisha ghadhabu kutoka rais huyo wa Uturuki
aliesema ari ya unazi imenea barani Ulaya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment