Wafanyakazi katika viwanja vya ndege mjini Berlin wamegoma kufanya
kazi wakidai kuongezewa mshahara hatua ambayo imesababisha mamia ya
safari za ndege kufutwa hii leo.Katika uwanja mkuu wa ndege wa Tegel
safari 455 zimefutwa wakati katika uwanja wa ndege wa Schoenefeld nje ya
mji huo wa Berlin safari nyingine za ndege 204 zimefutwa kwa mujibu wa
ripoti zilizochapishwa na shirika la habari la Ujerumani dpa hii leo.
Chama cha kutetea maslahi ya wafanyakazi Ver.di kimesema wafanyakazi
kiasi 2000 wa viwanja vya ndege wanaosimamiwa na chama hicho wamegoma
kuanzia alfajiri ya leo na mgomo huo utaendelea hadi kesho Jumamosi
alfajiri. Hatua hiyo imechukuliwa ili kuongeza shinikizo kwa waajiri
kuridhia kufanyika mazungumzo kuhusu kiwango kipya cha mshahara.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment