Umoja wa Ulaya na jumuiya ya mataifa ya Kusinimashariki mwa Asia
zimesema leo kuwa kanda hizo mbili zitajaribu kufufua mipango ya
makubaliano ya biashara huru kati yao, mnamo wakati mataifa ya Ulaya
yanatafuta njia za kunufaika na ukuaji imara wa eneo hilo. Umoja wa
Ulaya pamoja na jumuiya ya ASEAN yenye mataifa wanachama 10 ziliazisha
mazungumzo yenye lengo la kusaini mkataba wa kibiashara mwaka 2007
lakini mchakato huo uliwekwa kando miaka miwili baadae, ambapo Umoja wa
Ulaya uliamua kufanya majadiliano na nchi moja moja. Mazungumzo hayo
yamepata mafanikio mchanganyiko, ambapo mpaka sasa makubaliano
yamefikiwa na Singapore pekee na hivi karibuni Vietnam, lakini bado
hayajaanza kutekelezwa. Kamishna wa biashara wa Umoja wa Ulaya Cecilia
Mamstrom amesema iliamuliwa kati ya maafisa wa Umoja wa Ulaya na jumuiya
ya ASEAN leo, kuundwe mfumo kwa ajili ya kuanza upya mazungumzo, lakini
bado hakujawa na muda wa mazungumzo hayo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment