Mtanzania
Lilian Danieli mwenye kampuni yake ya NASHONA amefungua duka la nguo za
Kitanzania Goldsboro jimbo la North Carolina nchini Marekani. Uzinduzi
wa duka hilo ambalo lipo Center Street katikati ya mji huo wa Goldsboro
ulifanyika siku Jumamosi March 25, 2017. Anuani kamili ya duka ni 119
Center Street, Goldsboro, NC na simu ya dukani ni 918 947 1273.
Katika
duka hilo nguo mbalimbali vitenge toka Tanzania ikiwa asilimia 90
ameshona yeye mwenyewe na baadhi ya vingine kuja toka Tanzania. Duka
litakua linafunguliwa siku ya Jumanne mpaka Jumamosi. Picha na Vijimambo
Blog na Kwanza Production
Baadhi
ya wateja waliokuwepo dukani hapo siku ya uzinduzi wa duka hilo
Jumamosi March 25, 2017 Goldsboro, North Carolina nchini Marekani.
Lilian
Daniel Kulia akikinja moja ya nguo zilizo nunuliwa na mmoja ya wateja
wake siku ya uzinduzi wa duka lake la nguo za kiTanzania lililozinduliwa
siku ya Jumamosi March 25, 2017.
Kushoto ni Serena Danieli akisaidiana na dada yake Imani Danieli katika kuhakikisha mahesabu ya duka yanaenda sawa.
Lilian Danieli akiwa na mmoja ya wateja wake akiwaonyesha nguo zake na kuwapa maelekezo.
Mmoja ya wateja akilipia kitu alichonunua.
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi.
SHARE
No comments:
Post a Comment