Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati), Mkuu wa mkoa
wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo (wa kwanza kushoto), Mbunge wa
Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa pili kushoto), Mbunge wa Kibaha
Vijijini, Mhe.Hamoud Jumaa (wa nne kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala
wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Gissima Nyamo-hanga wakifurahia
uzinduzi wa mradi wa Usambazaji Umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA
III) katika mkoa wa Pwani. Hafla ya Uzinduzi huo ilifanyika katika
kijiji cha Msufini mkoani humo.
Na Teresia Mhagama
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, amezindua mradi wa
Usambazaji Umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) katika mkoa wa Pwani
ambao utawezesha vijiji mbalimbali katika mkoa huo kupata huduma ya Umeme.
Hafla ya Uzinduzi huo ilifanyika katika kijiji cha Msufini mkoani humo na
kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa mkoa wa Pwani,
Mhandisi Evarist Ndikilo, Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete na
Mbunge wa Kibaha Vijijini, Mhe.Hamoud Jumaa.
Uzinduzi wa mradi huo ulienda sambamba na utambulishaji wa Mkandarasi
atakayetekeleza sehemu ya kwanza ya Mradi huo ambaye ni kampuni ya Steg
International Services.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa Tatu kushoto), Mkuu
wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo (wa kwanza kulia), Mbunge wa
Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa pili kulia), Mbunge wa Kibaha
Vijijini, Mhe.Hamoud Jumaa (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa
Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Gissima Nyamo-hanga (wa
kwanza kushoto) wakifunua Jiwe la Msingi kuashiria uzinduzi wa mradi wa
Usambazaji Umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) katika mkoa wa
Pwani. Hafla ya Uzinduzi huo ilifanyika katika kijiji cha Msufini mkoani
humo.
Kabla ya uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA),
Mhandisi Gissima Nyamo-hanga alieleza kuwa Mradi wa Usambazaji Umeme
Vijijini wa Awamu ya Tatu unahusisha vipengele Mradi vitatu vya utekelezaji.
Alisema kuwa kipengele cha kwanza cha utekelezaji kitahusisha kufikisha umeme
kwenye vijiji ambavyo havijafikiwa kabisa na miundombinu ya umeme wa gridi na
kipengele cha Pili kitahusika na kuongeza wigo wa usambazaji umeme kwenye
vijiji ambavyo vimefikiwa na miundombinu ya umeme.
“Kipengele cha Tatu katika Mradi huu kitahusika na usambazaji wa nishati jadidifu
kwenye maeneo yaliyo mbali na gridi, ambayo ni vigumu kufikiwa na umeme wa
gridi yakiwemo maeneo ya Visiwa”, aliongeza Mhandisi Nyamo-hanga.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa Tatu kushoto), Mkuu
wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo (wa kwanza kulia), Mbunge wa
Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa pili kulia), Mbunge wa Kibaha
Vijijini, Mhe.Hamoud Jumaa (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa
Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Gissima Nyamo-hanga (wa
kwanza kushoto) wakifunua Jiwe la Msingi kuashiria uzinduzi wa mradi wa
Usambazaji Umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) katika mkoa wa
Pwani. Hafla ya Uzinduzi huo ilifanyika katika kijiji cha Msufini mkoani
humo.
Alisema kuwa Utekelezaji wa Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya
Tatu katika Mkoa wa Pwani utahusisha vipengele vyote vitatu na utatekelezwa
kwa vipindi viwili tofauti ambapo sehemu ya kwanza itahusisha upelekaji umeme
katika vijiji 204 kwa gharama ya Shilingi Bilioni 30.2 ambapo utekelezaji wa
sehemu ya kwanza umeanza Mwezi Februari 2017 na unatarajiwa kukamilika
Machi 2019.
Mhandisi Nyamo-hanga alitoa wito kwa wananchi watakaounganishiwa umeme
kukamilisha utandazaji wa nyaya katika nyumba zao mapema ili wakati
mkandarasi atakapofika katika maeneo yao, wawe tayari kulipia na kuunganishiwa
umeme.
Kwa upande wake, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Muhongo, alisema kuwa
utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini imefanyika kwa ufanisi kwani katika
mwaka 2007 ni asilimia 2.5 tu ya watanzania waishio vijijini walikuwa na umeme
lakini mpaka mwisho wa mwaka 2016, upatikanji wa umeme vijijini ulifikia
asilimia 49.5.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati), akikata
utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa Usambazaji Umeme vijijini wa Awamu
ya Tatu (REA III) katika mkoa wa Pwani. Wengine katika picha ni Mkuu wa
mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo (wa kwanza kushoto), Mbunge wa
Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa pili kushoto), Mbunge wa Kibaha
Vijijini, Mhe.Hamoud Jumaa (wa nne kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala
wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Gissima Nyamo-hanga.
Alisema kuwa, Watanzania wana haki ya kujivunia miradi hiyo inayofadhiliwa na
Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na kutekelezwa na TANESCO, kwani ni ya
kipekee duniani kutokana faida zake kwa wananchi wa vijijini ambapo gharama
mbalimbali zinabebwa na Serikali huku mwananchi akitakiwa kulipia shilingi elfu
27,000 ili aunganishiwe umeme.
Alisema kuwa, kwa kutambua umuhimu wa miradi hiyo, bajeti iliyotengwa kwa
mwaka wa Fedha 2016/17 ili kusambaza umeme vijijini ni zaidi ya shilingi
Trilioni moja.
Kuhusu hali ya Umeme katika mkoa wa Pwani, aliwaagiza watendaji wa
TANESCO na wataalam kutoka Ofisi ya Mkuu wa mkoa huo, kujadiliana ili
kufahamu mahitaji halisi ya umeme, hasa ikizingatiwa kuwa kuna viwanda
vinavyoendelea kujengwa na vilivyopo ambavyo vinahitaji si chini ya megawati
60.
Watendaji
kutoka kampuni ya Steg International Services wakimsikiliza Waziri wa
Nishati na Madini (hayupo pichani) wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa
Usambazaji Umeme Vijijini Awamu ya Tatu katika mkoa wa Pwani. Kampuni
hiyo itatekeleza sehemu ya kwanza ya Mradi huo wa Awamu ya Tatu.
Aidha, alitoa wito kwa wananchi kutodai fidia katika miradi ya Umeme, kutokana
na umuhimu wake katika huduma za kijamii kama vituo vya Afya, Shule,
majumbani na shughuli za kiuchumi ili kuleta mapinduzi katika maisha ya
wananchi hao.
Wabunge pamoja na Mkuu wa mkoa wa Pwani, walipongeza juhudi za usambazaji
umeme nchini zinazofanywa na Wizara ya Nishati na Madini, chini ya Profesa
Muhongo na kutumia fursa hiyo kueleza changamoto mbalimbali zinazopaswa
kushughulikiwa na Serikali ili wananchi pamoja na viwanda viweze kupata umeme
wa uhakika.
SHARE
No comments:
Post a Comment