Waziri
wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akiwa katika picha
ya pamoja na wadhamini wa Kikao kazi cha 12 cha Maafisa Mawasiliano wa
Serikali kinachofanyika Mkoani Dodoma.Kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu
wa Wizara hiyo Bi.Nuru Milao,Kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi
Bi.Elizabeth Kitundu,Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Dkt.Hassana
Abbas na Mwenyekiti wa TAGCO Bw.Innocent Mungy.
Na: Lorietha Laurence – WHUSM, Dodoma.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amewataka
Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini kuzisoma, kuzielewa na kuzifanyia
kazi sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 na ile ya Haki ya kupata Taarifa ya
mwaka 2016 ili kuweza kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi katika kuuhabarisha
umma.
Waziri Nape ameyasema hayo leo Mjini Dodoma alipokuwa akifungua mkutano wa
Maafisa Mawasiliano Serikalini ambapo licha ya kuwataka kuzijua sheria hizo pia
amewataka kuwa wabunifu kuendana na maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia
katika utendaji kazi wa kila siku.
Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akizungumza na
Maafisa Mawasiliano wa Serikali wakati akifungua kikao kazi cha 12 cha
Maafisa Mawasiliano wa Serikali kinachofanyika Mkoani Dodoma.
Aidha aliongeza kuwa kuwepo kwa sheria hizo mbili kutatengeneza daraja
litakalounganisha na kuwezesha utekelezaji wa majukumu ya Serikali kwa wananchi.
“Ni wajibu wa Maafisa Mawasiliano kuzijua na kuzitendea kazi sheria hizi ili
kurahisisha upatikanaji wa mawasiliano baina ya serikalini na umma hivyo kuondoa
ugumu uliokuwepo hususani katika kupatikana kwa taarifa muhimu kwa wananchi”
alisema Waziri Nape.
Aliongeza kwa kufafanua kuwa endapo utekelezaji wa sheria hizi mbili muhimu
utasimamiwa na kuzingatiwa basi kutakuwepo na matokeo chanya ya kiutendaji na
hivyo kuleta mafanikio makubwa yanayotarajiwa na umma.
Waziri Nape pia aliwataka Maafisa Mawasiliano hao kuwa wabunifu katika utekelezaji
wa majukumu yao kwa kuendana na maendeleo ya teknolojia ikiwemo matumizi ya
mitandao ya kijamii katika kuhabarisha umma na kutoa taarifa kwa wakati.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi.Nuru Milao
akiongea kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye kufungua rasmi Kikao
kazi cha 12 cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali kinachofanyika Mkoani
Dodoma tarehe 14 Machi 2017.
“Zama hizi sio zile za maafisa mawasiliano kujisifia kwa kuwa na safari nyingi badala
yake kuwa watekelezaji wa kazi zao kwa wakati na matokeo yanayoonekana kwa
umma ila kwa atakayeshindwa kutekeleza hayo basi tutaomba atupishe” alisema
Waziri Nape.
Aidha alieleza kuwa anafahamu kuwa kuna changamoto nyingi ambazo maafisa
mawasiliano wanakumbana nazo katika utendaji wao wa kazi ikiwemo ukosefu wa
vifaa ingawa si kigezo cha wao kutokutekeleza wajibu wao.
Katika kuhakikisha kuwa changamoto ya ukosefu wa vifaa inatatuliwa Waziri Nape
alitoa Wito kwa Makatibu Wakuu, Wakurugenzi na Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuweka
kipaumbele katika bajeti hii mpya kwa kutenga kiasi cha fedha ambacho kitasaidia
kununua vifaa kwa ajili ya Maafisa Mawasiliano wa Wizara, Taasisi, Mikoa, Wilaya na
Halmashauri .
Mkuu wa
Wilaya ya Bahi Bi.Elizabeth Kitundu akizungumza wakati wa ufunguzi wa
Kikao kazi cha 12 cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali kinachofanyika
Mkoani Dodoma.
Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi. Nuru
Millao alisema kuwa umuhimu wa mkutano wa Maafisa Mawasiliano Serikalini ni katika
kuwajengea uwezo wa kiutendaji pamoja na kutathmini utendaji kazi wao.
Kwa upande wake mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambaye ni Mkuu wa
Wilaya ya Bahi Mhe. Elizabeth Simon Kitundu ameishukuru Wizara kuandaa mafunzo
kwa Maafisa Mawasiliano Serikalini na kuyafanyia Mkoani Dodoma kwani kwa kufanya
hivyo itarahishisha mfumo wa kimawasiliano na kutangaza fursa zilizopo Mkoani
Dodoma hivyo kuwafanya watumishi wa umma kuwa na amani katika kutekeleza agizo
la kuhamia Dodoma.
Mkutano wa Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini umefanyika kwa mara
ya 12 huku lengo ikiwa ni kuwakutanisha kwa pamoja maafisa hao kutoka katika ngazi
mbalimbali za kiutendaji serikalini ikiwemo Wizara, Idara, Taasisi, Mikoa, Wilaya na
Halmashauri ili kuweza kubadilishana uzoefu wa kiutendaji pamoja na kutatua
changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO Dkt Hassan Abbas akichangia jambo
wakati wa kikao cha 12 cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali kinachofanyika Mkoani
Dodoma.
Maafisa Mawasiliano wa Serikali kutoka Wizara,Taasisi ,Halmashauri,Wakala na
Mashirika ya Umma,Tamisemi na Idara zinazojitegemea wakimskiliza kwa makini
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye(hayupo Pichani)
wakati akifungua Kikao kazi cha 12 cha Maafisa hao kinachofanyika Mkoani Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) akichangia
jambo wakati wa Kikao kazi cha 12 cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali
kinachofanyika Mkoani Dodoma.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akiwa katika
picha ya pamoja na Maafisa Mawasiliano kutoka Idara ya Habari-MAELEZO wakati wa
kikao cha 12 cha Maafisa hao wa Serikali kinachofanyika Mkoani Dodoma. Kulia kwake
ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi.Nuru Milao,Kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya
ya Bahi Bi.Elizabeth Kitundu,Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Dkt.Hassana
Abbas na Mwenyekiti wa TAGCO Bw.Innocent Mungy.
SHARE
No comments:
Post a Comment