Leo March 8 2017 ni siku ya Wanawake Duniani hivyo sio vibaya kama
tukicheki michango mbalimbali iliyofanywa na wanawake katika sekta
muhimu ya sayansi na teknolojia ambapo mara nyingi hutawaliwa na
wanaume. Nimekuletea list ya wanawake kumi waliyofanya uvumbuzi wa vitu
mbalimbali ambavyo vilibadilisha historia ya teknolojia duniani.
1:Florence Parpart. Mwaka
1914 Florence Parpart alivumbua friji la kisasa linalotumia umeme
ambapo uvumbuzi huo uliweka rekodi ya dunia hasa baada ya kuvumbuliwa na
mwanamke.
2: Marie Van Brittan. Anajulikana zaidi kwa mchango wake mkubwa katika uvumbuzi wa kamera za CCTV mwaka 1969, ambapo ugunduzi huu aliufanya baada ya kukithiri kwa uhalifu katika jiji la Newyork.
3: Stephanie Kwolek atakumbukwa
kwa uvumbuzi wake wa material yaliyotumika kutengeneza bullet proof,
vikoti ambavyo huvaliwa kwa ajili ya kuzuia risasi isiingie mwilini.
4: Hedy Lamarr: Ni mwafizikia aliyebobea katika maswala ya mawasiliano ambapo aligundua teknolojia ya wireless iliyosaidia kuanzishwa kwa wiFi na mfumo wa GPS.
5: Josephene Cochrane. Mwaka 1887 Josephene Cochrane alivumbua
machine ya kuoshea vyombo au dish washer ambazo alikuwa akiziuza
mahotelini mwaka mmoja baadae alifungua kiwanda chake.
6:Letitia Gee. Mwaka 1899 Letitia Geer alivumbua bomba la sindano na kubadilisha historia ya sekta ya afya.
7: Dr Maria Telkes mwaka 1947 alijenga nyumba ya kwanza duniani yenye mfumo wa umeme wa jua au solar energy.
8: Mwaka 1886 Maria Beasely alibuni
maboya ya kuogelea au life jackets baada ya kukithiri vifo vya baharini
ni uvumbuzi uliyopongezwa na watu wengi na kumfanya Maria Beasely kuwa mwanasayansi mwenye jina kubwa.
9: Dr Shirley Jackson ni
mwanafizikia aliyebuni nyaya au fiber cable zinazotumika leo hii kwenye
mitandao ya simu, pia uvumbuzi wake mwingine uliyomjengea jina ni
pamoja na machine ya fax, mfumo wa kusubirisha mtu kwenye simu au call
waiting.
10:Ada Lovelace: Unaweza usiamini lakini computer programmer wa kwanza duniani ni mwanamke Ada Lovelace alikuwa mtu wa kwanza kubuni program mbalimbali za computer.
SHARE
No comments:
Post a Comment