TRA

TRA

Wednesday, March 8, 2017

Mafuriko Dar: Watu kadhaa wamekwama kwenye maji Jangwani, wengine wapoteza maisha

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Mvua iliyonyesha leo Dar imeleta maafa sana kwani hadi sasa watu kadhaa wamekwama kwenye maji maeneo ya Jangwani Mto Msimbazi.

Jeshi la Uokoaji limeshafika na vifaa maalum vya uokoaji. Ila nashangaa Askari wengi wakiwa na bunduki na magwanda yao bila vifaa maalum
Screenshot from 2017-03-08 13-21-48.png
Boat inaandaliwa kuingizwa kwenye maji ili kuokoa watu

======

 

=> Hadi sasa mtu mmoja ameshaokolewa na Kikosi maalum cha uokoaji. wanatumia boat maalum inayojazwa upepo.
Moja2.jpg
=> Mwili uliotolewa kwenye maji ni wa Kijana kati ya Miaka 25 na 32. Sina uhakika sababu hayupo hai.
Jangwa.jpg
Kikosi Maalum cha Uokoaji kikiendelea na kazi

=> Kwenye maji haya ya Msimbazi kuna watu bado wanaonekana vichwa kwa mbali. Hatujajua hali zao zikoje. Ila shughuli ya Uokoaji inaendelea.

=> Helicopter ya Polisi inaimalisha ulinzi kwa juu huku ikiangalia kama kuna watu zaidi wamekwama majini
ndege.jpg Chopa ya Polisi
Chopa ya Polisi
16998686_1030827200395614_2797808922760516037_n (1).jpg17098445_1030827050395629_8220886967831850589_n.jpg

Kwa hali hii, bora mwaka huu Mvua isinyeshe Dar es Salaam Mwaka huu. Sababu leo Mvua ilinyesha kidogo tu lakini imeleta maafa. Je ikija kunyesha mvua kubwa itakuwaje?

Mungu atuepushie mbali balaa hili.

Naishauri Serikali kutumia mfano huu iwe fundisho kwao, Wazibue mitalo na sisi wananchi tuache kutupa vitu na uchafu kwenye mifereji ya maji.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger