Mbunge wa mafinga mjini Cosato Chumi akiongea na Wafanyabiashara wa mazao ya misitu wilayani Mufindi juu ya malamiko yao kwa TRA mkoa wa Iringa
Baadhi
ya wafanyabiashara wa mazao ya misitu wilayani Mufindi waliohudhulia
mkutano wa pamoja kati ya mbunge,TRA na wafanyabiashara.
Na Fredy Mgunda,Mufindi
Wafanyabiashara
wa mazao ya misitu wilayani Mufindi wamesema kuwa soko la mbao
limeshuka kwa kiwango kikubwa kutoka na mrundikano wa kodi katika wilaya
hiyo tofauti na wilaya nyingime.
“Ukienda
mbeya,njombe na maeneo mengine kodi ya vibali ni ndogo kuliko ya hapa
mufindi sasa tunataka kujua tatizo nini”walisema wafanyabiashara
Aidha
wafanyabiasha hao wameiomba mamlaka ya mapato mkoa wa iringa TRA kutoa
kibali cha usafirishaji kwa kuondoa usumbufu wa tozo za ushuru check
point na kuombwa lisiti za mashine kutoka kwa wakulima waliowauzia mbao
na nguzo.
Akizungumza
mmoja wa wafanyabiashara hao Zakayo Kenyatta Katika mkutano wa
wafanyabiashara wa mazao ya misitu na TRA alisema kuwa TRA wamekuwa
wasumbufu sana check point kwa kuwasimamisha zaidi ya siku tatu wakidai
lisiti hizo huku wafanyabiashara wakionyesha barua za watendaji kutoka
vijiji walivyonunulia zikikataliwa.
"Tunawaomba
TRA mkatoe elimu kwa mkulima mmoja mmoja kwa sababu ni ngumu sana
mkulima wa chini akuulizie nguzo 5 alafu awe na lisiti ya mashine kwa
hiyo tunawaomba TRA wakatoe elimu hiyo na kuwaamasisha wakulima hawa
Kuwa na hizo mashine kwani wakulima hao ni wale ambao wanauza miti yako
kutokana na matatizo mbali mbali walionayo na sio kampuni" alisema
Kenyatta
Akijibu
hoja hiyo meneja msaidizi WA TRA mkoa WA iringa Mustapha Mkilamwenye
alisema Kuwa wamekuwa wakiogopa kwenda kutoa elimu hizo kwa wakulima
kutokana na mkutano yao kuharibika kwa kuzomewa na kutokufikia muafaka
WA uelimishaji.
Pia
Mkilamwenye amewataka wafanyabiashara hao kupata kibari cha kununua na
kusafirisha kutoka TRA wilaya au mkoa kabla hqwqjaenda vijijini kununua
ili kukwepa uwumbufu huo check point.
"Ombi
lenu tumelipokea hivyo tunawaomba kabla hamjanunua mpate kibali kutoka
TRA mkoa au wilayani kuokoa usumbufu WA tozo za ushuru check point, pia
tutatoa elimu ya matumizi ya mashine kwa wakulima vijijini wauzapo miti
yako kwa wafanyabiashara" alisema
Kwa
upande wake Mbunge wa mafinga mjini Cosato Chumi alisema Kuwa ameamua
kuwakutanisha wafanyabiashara na TRA kupata ufafanuzi WA kuombwa ushuru
check point kutokana na kulalamikiwa na wafanyabiashara hao Kuwa magari
yako wamekuwa wakikaa check point zaidi ya siku tatu wakiombwa lisiti za
mashine kutoka kwa wakulima waliowauzia nguzo na mbao.
"Mkutano
huku ni mahususi kwa wrote tukipata ufafanuzi na kujua kwa nini
mnakamatwa check point na mkiobwa ushuru au njia kila mkoa,tra wanapaswa
Kuwa rafiki Wa wafanyabiashara na sio adui kwa sababu mufindi ndio
chanzo kikuu cha mapato ya nchi kutokana na zao LA mbao" alisema Chumi
Meneja
wa TRA wilayani ya Mufindi Filmoni Mwakapesile alisema Kuwa "ni kweli
tuhuma hizo na lawama tumezipata na tumekuwa tukipokea simu nyingi za
wafanyabiashara na kutatua matatizo yako lakini Leo tunashukuru Mbunge
amekututanisha na tumewapa uelewa na sisi kama TRA tumewaambia mini cha
kufanya kuondoa huo usumbufu"
SHARE
No comments:
Post a Comment