Mjumbe
wa bodi ya wakurugenzi ya TCCIA Investment PLC bi Magdalena Mkocha
akizungumza na wafanyabiashara mkoani Lindi katika ukumbi wa Double M
humo.Bi
Mkocha alisema TCCIA Investment ilianzishwa mwaka 2005 ikiwa na mtaji
wa shilingi Bilion 1.97 imeweza kukuza mtaji hadi zaidi ya Bilion 28.6
na imekuwa ikilipa gawiwo kwa wanahisa wakeMkochi
ameongeza kuwa TCCIA Investment PLC ni kampuni ya uwekezaji wa pamoja,
imara na imekuwa ikifanya vizuri sana hivyo amewahimiza wajasiriamali
hao kuitumia fursa hii muhimu na adhimu kabla ya March 14 mwaka 2017,
ambapo milango ya uuzaji wa hisa hizo itafungwa
Mjumbe
wa bodi ya wakurugenzi ya Chemba ya Biashara,viwanda na kilimo,
Magdalena Mkocha, amewataka wananchi na wafanyabiashara wa Mikoa ya
Lindi na Mtwara kujitokeza kwa wingi na kuchangamkia fursa ya soko la
hisa za TCCIA Investment PLC kwa awamu ya awali ambayo inakaribia
kuisha.
Hayo
ameyasema wakati akizungumza wafanyabiashara kwenye ziara yake ya mikoa
ya kusini, Lindi na Mtwara alipokuwa kwenye mikutano ya kuhamasisha
ununuzi wa Hisa hizo ambazo zinamilikiwa na kampuni hiyo.
Bi Magdalene Mkocha akifafanua jambo kwa wafanyabiashara waliohudhulia mkutano huo mkoani Lindi
“Nipende
kuwahimiza ndugu zangu tuchangamkie fursa hii kwasababu TCCIA
Investment PLC nikampuni imara ambayo imeweza kusimama na kujiendesha
yenyewe kwa kipindi kirefu bila kutegemea mikopo, sasa imeona ni wakati
sasa kuwapa na wananchi nafasi ya kushiriki katika kuchangia mitaji yao
ili mwisho wa siku wavune matunda kupitia hisa zao” alisema Bi Mkocha
Mmoja
wa wajasiriali waliohudhulia mkutano huo Bwana Condrad Makwiya akiuliza
swali kwa bi Mkocha kuhusiana na upatikanaji wa hisa hizo
Hisa
za TCCIA Investment PLC zinapatikana kwa shilingi 400 tu, huku kima cha
chini cha kununua hisa hizo kikiwa ni hisa 100, pia unaweza kupata hisa
hizo kupitia kwa mawakala wa walioidhinishwa na Mamlaka ya Masoko ya
Mitaji na Dhamana (CMSA) au tembelea kwenye matawi yoyte ya Benki ya
CRDB.
Pia unaweza kutumia simu ya mkononi kwa kupiga *150*36# kisha kufuata maelekezo.
Bi
Madgalena Mkocha akigawa vipeperushi kwa wafanyabiasha mkoani Mtwara
baada ya kumalizka kwa mkutano huo kulia kwake ni Makamu Mwenyekiti
TCCIA Mkoa wa Mtwara.
Moja ya mshiriki mkoni Lindi akitoa shukrani zake kwa uongozi wa TCCIA Investment PLC kuhusu fursa hiyo uuzaji wa hisa
SHARE
No comments:
Post a Comment