Shaban Njia, KAHAMA
KATIKA kuhakikisha Mkoa wa Shinyanga unaweza kufanya vema katika matokeo ya mitihani ya kumaliza kidato cha nne kwa Wananfunzi wa kike, Kampuni ya Acacia kupitia mgodi wake wa Dhahabu wa Bulyanhulu umeanza programu ya kuwazadia wanafunzi hao zawadi pindi wanapofanya viruzi katika masomo mbalimbali.
Zawadi hizo zitakuwa zikitolewa kila mwaka katika Maazimisho ya Siku ya Wanawake Duniani na tayari kwa mwaka huu imewapatia Baskeli jumla ya wanafunzi wa kike nane na walimu walezi wawili katika shule za sekondari za Bugarama na Bulyanhulu waliofanya vizuri katika masomo yao.
Akikabidhi baiskeli hizo juzi, Ofisa uhusiano wa mgodi huo, Zuwena Sekondo alisema kuwa baskeli hizo zitasaidia kuwatia hamasa wananfunzi wa kike hasa wale wanatumia umbali mrefu kutoka majumbani kwao kwenda shule kuendelea kufanya vema katika mitihani ya shule pamoja na ile ya kitaifa.
Sekondo aliwataja waliozawadiwa Baskeli hizo katika Sekondari Bulyanhulu ni Irene Jimmy wa kidato cha tatu aliyeshika nafasi ya kwanza katika mitihani wa kidato cha pili mwaka jana,huku Zainabu Kisambale wa kidato cha tatu akifanya vizuri katika mihati yake ya kidato cha pili kwa kupata daraja la pili.
Wengine ni Maombi Silvester aliyeshika nafasi ya kumi katika mitihani yake na kuendelea kuonesha nidhamu huku Rehema Abdallah wa kidato cha nne akishika nafasi ya kumi katika mitihani ya shule na pia mwaka jana akiwa kidato cha tatu alishika nafasi ya tatu.
Aidha Sekondo aliendelea kuwataja wanafunzi wa kike walipata baskeli katika sekondari ya Bugarama kuwa ni Jeschal Peter kidato cha kwanza anaefanya vizuri katika somo la kingereza ,Rozi Juma Omary kidato cha pili aliyeshika ya kumi katika mitini wa kitaifa mwaka jana.
Pia Ofisa Maendeleo huyo aliwataja pia Philomena Achoro kidato cha pili aliwahi kushika nafasi ya kwanza akiwa kidato cha kwanza mwaka jana,Evelini Silasi kidato cha nne aliwahi kushika nafasi ya sita akiwa kidato cha tatu mwaka jana pamoja na mwalimu wao mlezi Priscal Mwanantemi.
Hata hivyo, aliyataka mashirika ya kiserikali na yale yasiyo ya kiserikali kujitoa katika kumpigania mtoto wa kike katika kupata elimu hali ambayo isaidia mtoto wa kike kujiongoza katika maisha yake ya baadae nakuongeza kuwa kutasaidia kupunguza wimbi la wanawake wasio na elimu.
Katika hatua nyingine, Kampuni ya Acacia imetoa mashuka, , sabuni, dawa ya meno pamoja na mafuta kwa wagonjwa wa Wanawake na Wanaume katika kituo cha Afya cha Bugarama na Lunguya lengo likiwa ni kupambana na wimbi la uchafu katika vituo vya afya katika Halmashauri ya Msalala.
Ofisa tabibu kutoka katika kituo cha afya cha Lunguya, John Malango alisema kuwa kutokana na msaada uliotloewa na mgodi wa Bulyanhulu utasaidia kuboresha huduma ya usafi wa mazingira ya kituo hicho na kuwataka watu wengine kujitokeza katika kuboresha huduma za kiafya.
SHARE
No comments:
Post a Comment