Marekani inapiga
marufuku vifaa vya kielektroniki kuingia katika ndege kutoka mataifa
manane ya mashariki ya kati na Afrika Kaskazini.
Vyombo vya habari nchini humo vinasema kuwa agizo hilo lilisababishwa na ujasusi uliokusanywa ughaibuni.
Vifaa hivyo vitashirikisha Laptopu, kamera za tabiti [tablet], vifaa vya kuchezesha kanda za video pamoja na zile za michezo ya kielektroniki lakini simu hazikutajwa.
Idara ya usalama wa ndani ulikataa kutoa tamko lolote kuhusu swala hilo na inatarajiwa kuzungumza siku ya Jumanne.
Mnamo mwezi Februari ndege inayosimamiwa na kampuni ya ndege ya Daallo nchini Dubai iliharibiwa na mlipuko muda mchache baada ya kuanza kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Mogadishu nchini Somalia.
Uchunguzi umesema kuwa abiria mmoja ambaye alitolewa katika ndege hiyo alikuwa amebeba laptopu yenye bomu.
Rubani alifanikiwa kutua huku mshambuliaji huo akiwa ndiye aliyefariki pekee.
Iwapo bomu hilo lingelipuka ndege hiyo ikiwa juu sana, ndege hiyo ingeharibika vibaya.
Kundi la wapiganaji wa Alshabab ambalo linashirikishwa na kundi la al-Qaeda limedai kuwa lilihusika na kwamba kuna uwezekano wa mashambulio mengine swala linalowatia wasiwasi wapelelezi wa Marekani.
Lakini maafisa wamekataa kuelezea kinaga ubaga kwa nini marufuku hiyo imewekwa.
SHARE
No comments:
Post a Comment