TRA

TRA

Tuesday, March 21, 2017

Umoja wa Ulaya na Libya kuukabili uhamiaji

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
Mawaziri wa mambo ya ndani wa nchi za Umoja wa Ulaya na eneo la Afrika Kaskazini wameahidi kupambana na biashara ya usafirishaji wa binadamu kutoka Libya huku kukiwa na ongezeko kubwa la watu wanaojaribu kuingia Ulaya. 

Wanadiplomasia wa mataifa hayo walikutana jana mjini Roma, Italia na kutoa taarifa ya pamoja kuahidi kuongeza ushirikiano na kupeana taarifa katika jitihada ya kuzitafutia ufumbuzi sababu hasa za uhamiaji, pamoja na kuzuia usafirishaji wa watu na kuilinda mipaka.

 Serikali ya Libya inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa imeomba msaada wa vifaa vya thamani ya euro milioni 800, zikiwemo helikopta, boti, rada na magari, kusaidia kupunguza idadi ya wahamiaji wanaoingia Ulaya kupitia baharini na nchi kavu.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger