Uturuki imesema itasimamisha uhusiano wa ngazi ya juu wa kidiplomasia
na Uholanzi, baada ya Uholanzi kuwazuia mawaziri wa Uturuki kufanya
mikutano ya hadhara na waturuki waishio Uholanzi. Naibu Waziri Mkuu wa
Uturuki Numan Kurtulmus amesema ndege zinazowasafirisha wanadiplomasia
wa Uholanzi hazitaruhusiwa kuruka katika anga ya Uturuki. Hali
kadhalika, balozi wa Uholanzi nchini Uturuki ambaye yuko nchini mwake
kwa mapumziko, amearifiwa haruhusiwi kurudi nchini Uturuki. Kurtulmus
amesema hadi pale Uholanzi itakapokuwa imelipa kwa namna fulani yale
iliyoyafanya, hakutakuwa na mikutano kati ya maafisa wa nchi hizo,
kuanzia mawaziri kwenda juu. Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan
ameituhumu serikali ya Uholanzi kujifanya kama masalia ya wanazi. Rais
huyo anatafuta uungwaji mkono wa waturuki waishio nje, katika kura ya
maoni inayotarajiwa kumpa rais madaraka ya mkubwa wa nchi. Waziri Mkuu
wa Uholanzi Mark Rutte amesema vikwazo hivyo vya Uturuki sio vibaya
sana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment